Wafanyikazi wa usafiri wa mjini Sao Paulo wamepiga kura
kuidhinisha mgomo wao uendelee kwa mda usiojulikana licha ya uamuzi wa mahakama
ya leba nchini humo, iliyokuwa imewaamuru wafanyikazi hao kurudi kazini mara
moja.
Koti ilikuwa imesema wakuu katika vyama vya wafanyikazi hao wa usafiri wa mjini Metro, walikuwa wametumia mamlaka yao vibaya kwa kuanzisha mgomo tangu alhamisi iliyopita.
Maandamano mengi yamekuwa yakulalamikia hali ngumu ya usafiri
lakini sasa wafanyikazi wa treni za mijini ziitwazo Metro ndio waliogoma kutaka
nyongeza ya mishahara.
Huku nusu ya vituo vya usafiri vikiwa tayari vimefungwa, msongamano wa magari
umezidi kuizonga Sao Paulo.
Sasa wasiwasi unaongezeka, wa Je hali ikiendelea hivyo itakuaje hapo alhamisi
wakati jiji hilo ndilo linafungua dimba hilo?
Wafanyikazi hao wanadai nyongeza ya mshahara ya asilimia 12 ilhali serkali
imesema itamudu nyongeza ya takrban asilimia 9.
wengi wa wasafiri hulalamikia msongamano na gharama za juu za usafiri nchini
Brazil
Chanzo BBC
0 comments :
Post a Comment