Itakumbukwa tarehe 16/06/2013 ilikuwa ni siku ya uchaguzi mdogo wa
madiwani kwa baadhi ya kata nchini. Uchaguzi huo umefanyika kwenye kata
ishirini na mbili (22) -kati ya kata ishirini na sita (26)
zilizotangazwa kufanya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi wazi.
Matokeo tuliyoyapata toka kwenye maeneo yaliyofanya uchaguzi
yanaonyesha kuwa kati ya kata 22 zilizofanya uchaguzi CCM tumeshinda
kata 16 sawa na asilimia 72.72% na wenzetu wamechukua kata 6 zilizobaki
sawa na asilimia 27.28%.
Tunawashukuru sana kote walikoonyesha imani yao kubwa kwa Chama chetu
kwa kutupa dhamana ya kuendelea kuwatumikia. CCM inawaahidi utumishi
uliotukuka.
Hata wale 27.28% walioamua
kuwajaribu wenzetu, tunawatakia kila lakheri, kwani wametumia haki yao
ya kidemokrasia kuchagua wanaodhani watawasaidia kufikia malengo yao ya
kimaendeleo. Uchaguzi kwenye kata hizi zote umeisha sasa tuwatumikie
wananchi.
Kata nne za jiji la Arusha hazikufanya uchaguzi baada ya kuahirishwa
kufuatia tukio la kusikitisha la kulipuka kwa bomu kwenye mkutano wa
kampeni wa Chadema mjini Arusha tarehe 15/06/2013.
CCM tunalaani tukio hilo la mlipuko wa bomu na matukio yanayofanana na
hayo katika nchi yetu. Tunawapa pole wale wote walioathirika na tukio
hilo.
Ni vizuri serikali ikalichunguza
swala hili kwa kutumia muda mfupi na kuhakikisha waliohusika
wanapatikana na kuchukuliwa hatua zinazostahili.
Pamoja na kulaani na kuitaka serikali kukomesha vitendo hivi nchini, ni
wakati muafaka kwa vyama vya siasa nchini kujitazama upya kwani kuna
kila dalili kuwa tukio hili kama alivyonukuliwa na baadhi ya vyombo
vya habari mhe. Mbowe Mwenyekiti wa Chadema Taifa kuwa ni la kupangwa,
inawezekana limepangwa na Chadema wenyewe.
Hali ya kisiasa jijini Arusha kuelekea uchaguzi huo ilikuwa wazi kuwa
wana Arusha walishaamua kuzirudisha kata hizo nne kwa CCM, hasa baada ya
kuchoshwa na maandamano na vurugu za kila siku jijini Arusha.
Aidha kauli za kukata tamaa za
viongozi wa Chadema na vitendo vyao ni dalili tosha kuwa tukio hili
lilipangwa na Chadema wenyewe.
Home
»
»Unlabelled
»
CCM WAWASHUTUMU CHADEMA KWA BOMU LA ARUSHA
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment