“Kifo cha Ngwair, kilivuta makundi mbalimbali kushiriki kwa hali na mali
kuchangia na kumzika, taifa lilizizima mkoa kwa mkoa, mguso huo wa
kitaifa aliokuwa nao mwanamuziki huyo, Ommy hakuuona, isipokuwa akanena:
‘Sitaki kufa maskini kama Ngwair’ limeandika gazeti hilo.

Ommy amekanusha kusema kauli hiyo na kudai kuwa habari hiyo imeandikwa
baada ya kushindwa kuelewana malipo ya show waliyomtaka akatumbuize.
“Watu wa Global Publisher wana tamasha lao la Matumaini, kwahiyo
wakanipigia simu wakataka nifanye nao show kwahiyo tukawa tunabargain
kuhusu bei. Wakati tunabargain kuhusu bei nikawa nimewaambia kwamba mimi
nahitaji kiasi fulani, tukabishana bishana, mwisho wa siku
hatukuafikiana. Baada ya pale wakakata simu, matokeo yake limekuja
kutoka hilo gazeti,” amesema Ommy.
Ameongeza kuwa gazeti hilo limetumia kauli aliyoisema siku ya KTMA 2013
aliposema kuwa amechoka kuona wasanii wanakufa maskini wakati kuna
makampuni mengi yanayoweza kuwapa mikataba na kufanya nao kazi ili wawe
na maisha mazuri.
“Kwa mtu anayenifahamu kama Ommy na watu ambao wamefanya kazi na mimi
wananielewa vizuri lakini ukiangalia habari yao nzima imekaa katika
misingi ya kiuchochezi. Wao wameamua kinichafua sababu tulikuwa tupo
kwenye mazungumzo ya kibiashara na hatukuafikiana.”
Ameongeza kuwa wakati wamempigia simu mara ya pili walikuwa wakimuuliza maswali ili kutengeneza majibu ya kumchafua baadaye.
“Kwanza mimi ni muislamu, najua hata maiti akishakufa jinsi ya
kumuongelea kwahiyo wao walikuwa wananitengenezeshea kauli. Nikasema
hapana, mimi nilichozungumza ni kwamba kama kweli tunataka tuendelee na
hii sanaa basi ninyi pia muwe mifano mizuri ya kutulipa vizuri kwasababu
tunatumia nguvu nyingi kuinvest.”
Kwa upande wa Mkurugenzi mkuu wa Global Publisher, Abdallah Mrisho
amekanusha kuwa gazeti la Ijumaa halijaandika habari hiyo kwa nia ya
kumchafua ama kumkomoa Ommy baada ya kushindwa kuafikiana bei ya kumlipa
kwenye tamasha la Matumaini. Mrisho amesema tamasha la Matumaini
linaandaliwa na menejimenti tofauti ambayo haihusiani na masuala ya
editorial.
“Labda issue ingekuwa story iliyoandikwa si ya kweli labda issue ndio ingekuwa hapo,” Mrisho alisema
0 comments :
Post a Comment