
MR KUMUHANDA
Dar es Salaam. Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema amefanya mabadiliko ya makamanda na wakuu wa Upelelezi wa Jinai, huku Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda akirejeshwa makao makuu ya jeshi hilo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa
Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso nafasi ya Kamuhanda, ambaye hivi
karibuni alipandishwa cheo na kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP),
inachukuliwa na Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP), Ramadhani Mungi ambaye alikuwa Makao Makuu ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai.
Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa Maalumu wa
Kinondoni, Charles Kenyela amehamishiwa Makao Makuu na atakuwa kwenye
Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai na nafasi yake inachukuliwa na
aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa wa Arusha (ACP),
Camilius Wambura. Taarifa hiyo ilieleza zaidi kuwa, DCP Ally Mlege
aliyekuwa Makao Makuu ya Polisi amehamishiwa Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam kuwa Mkuu wa Utawala na Rasilimaliwatu.
Aidha, taarifa hiyo ilieleza kuwa, ACP Duwan
Nyanda, ambaye yuko Makao Makuu ya Upelelezi atakuwa Mkuu wa Upelelezi
wa Makosa ya Jinai wa Arusha.
Kamuhanda na Mwangosi
Wadau wa sekta ya habari na wanaharakati
hawatamsahau Kamuhanda alipokuwa Kamanda wa Mkoa wa Iringa kutokana na
tukio la Septemba 2, mwaka jana wakati polisi mkoani humo walipomuua
Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel Ten, Daudi Mwangosi katika
Kijiji cha Nyololo.
0 comments :
Post a Comment