Mirerani. Kufuatia vitendo vya kigaidi
vinavyoendelea nchini, Mkuu wa Kituo cha Polisi Mirerani wilayani
Simanjiro mkoani Manyara, Ally Mohamed Mkalipa ametoa wito kwa viongozi
wa madhehebu ya dini wa mji mdogo huo kuanzisha vikundi vya amani na
ulinzi katika maeneo yao.
Akizungumza juzi na viongozi wa madhehebu ya dini
wa mji mdogo wa Mirerani, Mkalipa alisema lengo la kuanzisha vikundi
hivyo vya watu watano ni kuhakikisha uwapo wa amani kupitia ulinzi na
usalama katika maeneo ya ibada.
Alisema baada ya viongozi wa madhehebu kwenye
makanisa na misikiti kuchagua watu watano watakaounda kikundi cha ulinzi
na usalama kwenye maeneo yao, amani na usalama itakuwapo kwenye wa
nyumba hizo za ibada.
“Wanaweza kuweka ulinzi usio na bughudha kwa
waumini, lakini watakuwa wanachukuwa tahadhari endapo kuna mtu amebeba
kitu ambacho siyo cha kawaida, katika sehemu za ibada ili kibainike ni
kitu gani,” alisema Mkalipa.
Alidai kuwa endapo kikundi cha watu watano
kitakuwa kinafanya ulinzi kwenye maeneo ya madhehebu, amani na usalama
itakuwepo na endapo kutakuwa na tukio lolote hatarishi,watatoa taarifa
kituo cha polisi au kwa maofisa watendaji.
Pia, aliwataka viongozi hao wa madhehebu kutoa taarifa ya ujio wa ugeni nyeti katika eneo hilo.JE WATAFANIKISHA KWA HILOOO.....toa maoni yako
0 comments :
Post a Comment