Hatua ya Ronaldo kusema hajafanya mazungumzo ya kuongeza mkabata na Real Madrid, kumefungua njia ya kurudi Ligi Kuu England.
Madrid, Hispania. Cristiano Ronaldo amezidi
kufungua njia ya kurejea Manchester United ya England baada ya juzi
kusema hatima ya kuendelea kubaki Real Madrid ya Hispania iko shakani.
Kadhalika, amesema mazungumzo juu ya kuongezewa
mkataba mpya Hispania, hayajafanyika tofauti na ilivyoelezwa awali na
Rais wa Madrid.
United imekuwa ikifanya kazi kwa nguvu kujaribu
kumsajili winga huyo hatari kwa ada ya Pauni 60 milioni wakati wa
usajili wa majira ya joto.
Ilianza kutengeneza mpango huo tangu Februari mwaka huu.
Katika pesa hiyo ya usajili, United pia inataka
kumlipa mshahara wa Pauni 250,000 pamoja kumwongezea mikataba ya
wadhamini wa klabu kama Kampuni ya magari ya Chevrolet na Nike.
Wiki jana, Rais wa Madrid, Florentino Perez
alisisitiza kwa kusema Ronaldo atapewa mkataba mpya kabla ya kuanza
msimu mpya wa ligi ya Hispania.
Pia alisisitiza dhamira yake ya kumfanya kuwa
miongoni mwa wachezaji wanaolipwa vizuri duniani, akijitapa pia kumfanya
amalize kucheza soka akiwa na klabu hiyo ya Hispania.
Lakini mwenyewe Ronaldo, ambaye hana kawaida ya
kujipeleka kwenye vyombo vya habari na kuongea, alisema hakuna
mazungumzo yoyote ya kumwongezea mkataba yaliyofanyika mpaka sasa kwenye
Uwanja wa Bernabeu.
Nyota huyo wa Kireno: Alisema: “Habari zangu zote zinazosikika kuhusu kuongeza mkataba mpya Madrid, hazina ukweli.”
Hatua ya Ronaldo kueleza jambo hilo, inachukuliwa
kuwa siyo ya kawaida hasa kwa kuzingatia kuwa kwa siku za karibuni
amekuwa kimya kuhusu hatima yake Madrid.
Ronaldo amecheza misimu minne kwenye Uwanja wa
Bernabeu, akifunga mabao 201 katika mechi 199 za mashindano yote na
kuisaidia klabu hiyo kutwaa taji la La Liga mwaka 2012.
0 comments :
Post a Comment