TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Kijana aliyejulikana kwa jina la Daudi Lefi Mkazi wa Shinyanga ameshambuliwa na walinzi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga (SUMA JKT) wanaodaiwa kumtaka aondoke wodini kwamba muda wa kusalimia wagonjwa umeisha ili hali akisubiri kupatiwa gharama za dawa kwa ajili ya mgonjwa wake  

Akisimulia kuhusu tukio hilo, ndugu wa kijana huyo, Lydia Lefi amesema kuwa kaka yake amekutwa na mkasa huo wakati akiwa katika harakati za kulipia dawa za mama yao ambaye amelazwa katika hospitali hiyo jana Januari 21,2021. 

Daudi Lefi amesema walinzi hao  walidhani amefika muda huo huo hospitalini wakati yeye alikuwa  amefika hospitalini hapo muda mrefu lakini Computer za Hospitali zikawa hazisomi jina la mgonjwa wake wakati anataka kununua dawa.

Baadhi ya wagonjwa na watu wanaouguza wagonjwa wameeleza kusikitishwa na kitendo cha walinzi hao kumpiga ngumi na mkanda na kuongeza kuwa baadhi ya walinzi katika hospitali hiyo wana lugha mbaya na wanatumia ubabe hawaangalii utu.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga, Dr  Luzila John Boshi amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa atatoa taarifa baadae. ANGALIA MKASA MZIMA HAPA

0 comments :

 
Top