Mwanamuziki Kanye West amekubali kuandikishiana hati ya makubaliano kabla ya ndoa (Prenup)na miongoni mwa mambo ambayo atakuwa akimfanyia mpenzi wake Kim Kardashian ni pamoja na kumlipa Dola milioni moja kila mwaka katika kipindi chote cha ndoa yao.
Kwa mujibu wa radar online Kanye pia atamuachia Kim nyumba yao mpya iliyopo Bel Air Los Angeles, ambayo imeandikwa jina la mwanamama huyo. vilevile fedha zote zitakazopatikana kupitia Kim, ikiwemo matangazo ya kipindi cha "keeping with Kardashian" zitaendelea kuwa za Kim.
Shinikizo hilo lilitokana na mama wa Kim kumtaka Kanye kukaa mbali na shughuli za kifedha za binti yake, kwa madai kuwa anaingilia maisha binafsi ya mwanaye badala ya mapenzi
0 comments :
Post a Comment