Kwa muda mrefu sana, Madai ya wanawake wa Tanzania yamekuwa katika kuhakikisha kuna ushiriki sawa kwenye ngazi mbalimbali za maamuzi nchini. Katika Rasimu ya Pili ya Tume ya Katiba. (Tume ya Warioba) Wanawake walihakikishiwa usawa wa uwakilishi Bungeni. Rasimu ilisema yafuatayo.
Ibara 113 (3)“Katika Kila Jimbo la Uchaguzi, Kutakuwa na nafasi mbili zaubunge, moja kwa ajili ya mwanamke na moja kwa ajili ya mwanaume. Kwa mantiki hii wanawake walihakikishiwa asilimia 50 kwa 50 kwenye ngazi ya ubunge.
Katiba Pendekezwa ya Bunge la Katiba imetupilia mbali kilio cha wanawake nchini. Imefuta uwakilishi wa 50 kwa 50 kwenye ngazi ya ubunge. Ibara ya 129 (4) “Bila kuathiri masharti ya Ibara hii, msingi wa uwakilishi katika ibara ndogo ya (2) (a), UTAZINGATIA uwakilishi ulio sawa kati ya wabunge wanawake na wanaume”
1. Neno KUZINGATIA hapa linaleta shida. Kifungu hiki hakilazimishi upatikanaji wa uwakilishi sawa katika ngazi ya ubunge kati ya mwanamke na mwanaume. Kuzingatia sio kuhakikisha.
2. Pia kifungu hiki kimeshindwa kuainisha namna upatikanaji wa usawa wa wanawake utakavyokuwa.
3. Ukiangalia idadi ya wabunge wote watakaoingia bungeni, upatikanaji wa 50 kwa 50 ni mgumu. Rasimu inampa Raisi nguvu za kuteua wabunge watano toka kwenye kundi la watu wenye ulemavu. Nusu ya 5 ni mbili na nusu. Umewahi kuona watu mbili na nusu?
4. Kuna wabunge wengine watawakilisha kwa kupitia tiketi mbalimbali, kama Spika na Mwanasheria mkuu. Hawa wanaweza kufanya idadi ya uwakilishi isifike 50 kwa 50.
Hivyo tunadhani bado wanawake wa Tanzania hawajasikilizwa kilio chao cha muda mrefu na ndio hasa sababu ya kwanza ya kupinga KATIBA PENDEKEZWA. Kwa sababu maoni ya wanawake ambao ni idadi kubwa ya wananchi yamepuuzwa.
Wakati Tunasubiri Mambo 39 mazito yaliyobaki, Kwa umoja wetu tulitafakari hili. Namna ya Kushiriki. Changia mada,toa maoni yako, wakaribishe marafiki na watanzania wenzako wajue kinachoendelea na wao washiriki, sambaza ujumbe huu kwa wengine, share, invite, like and comment
0 comments :
Post a Comment