
Ndege ndogo aina ya Learjet 36 ilipata ajali mida ya saa 11:10 jioni siku ya jumapili na kusababisha vifo vya watu kadhaa akiwemo aliyekuwa mhamasishaji Myles Munroe, Mke wake na watu wengine waliokuwemo ndani ya ndege hiyo.
Idara ya usafiri wa anga ya Bahama imesema kuwa ndege hiyo ilipata ajari ilipokuwa inajiandaa kutua katika uwanja wa Bahama International Airport. Msemaji wa idara hiyo Burrows amesema kuwa ndani ya ndege hiyo kulikuwa na watu wachache wakiwemo marubani wawili na hakuna aliyetambuliwa baada ya ajari hiyo..
Pia ndani ya ndege hiyo kulikuwa na Mchungaji Richard Pinder, ambaye ni kati ya viongozi wa umoja wa makanisa ya kiinjiristi na alijjulikana kwa huduma zake za kiroho.
Munroe mwenye umri wa miaka 60 ni mhubiri wa kimataifa na mhamasishaji wa masuala mbalimbali yakiwemo ya kiuchumi, kisiasa pamoja na kijamii
Aidha Munroe ameandika vitabu mbalimbali zaidi ya vitabu 100 vinavyohusu uhamasishaji, ambavyo vilikuwa vikiuzwa zaidi katika mataifa yanayoendelea kama vile nchi za Caribbean na Afrika.
Burrows amesema kuwa ndege hiyo ilikuwa inaelekea nchini Bahama katika mkutano wa viongozi wa Global Leadership Forum ambao uliandaliwa na taasisi ya Munroe's kufanyika siku ya alhamisi. Taasisi hiyo imetoa taarifa akuwa mkutano huo utaendelea japo kwa ufupi kwa kuwa ndivyo Dr. Munroe alipenda itimie hivyo.
Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehem..........
The aviation ministry said it would begin a full investigation at daybreak Monday.
0 comments :
Post a Comment