TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


Rais Xi JinPing wa Uchina alizuru nchini tanzania mwaka uliopita

Inadaiwa kuwa wanunuzi, raia wa Uchina walinunua maelfu ya kilo za pembe za ndovu nchini Tanzania na kuzitorosha kutoka nchini humo kupitia ndege ya kibinafsi ya raia wa Uchina Xi Jinping,wakati alipozuru bara Afrika.
Kwa mujibu wa shirika la ujasusi la mazingira lililo na makao yake mjini London.
Pembe hizo zilinunuliwa wiki moja tu kabla ya ziara ya rais  wa Uchina kuingia nchini tanzania mwaka ulioipita(2013) ambapo zilifichwa katika mifuko ya wanadiplomasia ili kutokamatwa.

Pembe za ndovu

Shirika hilo pia linadai kwamba wajumbe waliokuwa wakiandamana na Rais Xi walinunua viwango vikubwa vya pembe hizo.
Uuzaji wa Pembe za ndovu ulipigwa marufuku mwaka 1989 ili kuwazuia wawindaji haramu kuwaua ndovu.
kumekuwa na shutma za ujangiri katika mataifa ya Africa yenye idadi kubwa ya ndovu ambao wamekuwa wakiwindwa na mataifa yaliyoendelea kiuchumi.
pamoja na kuwepo kwa kampeni ya tokomeza ujangiri ambayo ilaumiwa na watanzania wengi miezi kadhaa iliyopita , sasa hofu inazidi kutanda baada ya shehena ya meno ya ndovu kukamatwa tena.

0 comments :

 
Top