TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Mshambuliaji wa Liverpool anayekipiga klabu ya Lile ya Ufaransa Divock origin, anajiandaa kutua Anfield Januari mwakani baada ya taratibu za kuvunja mkataba wake kuanza kufanywa na klabu ya Liverpool.

Liverpool watalazimika kulipa pauni 5 milioni, huku klabu ya Lile ikiwa imeanza taratibu za kumnasa mshambuliaji Jozi Altidore kwa ajili ya kuziba pengo la Origi.

Origi #17 akiwa kazini
Majogoo hao wa Anfield walimnunua kinda huyo kutoka Lille, na kumwacha huko kwa mkopo wa mwaka mmoja, lakini sasa itawalazimu kuvunja mkataba huo ili wazibe pengo kubwa lililoachwa katika safu ya ushambuliaji baada ya Daniel Sturidge kuumia, na Mario Balotelli kushindwa kuonyesha makali yake msimu huu.

Origi tayari ametumbukiza magoli matatu na kutengeneza nafasi Tisa za kufunga, kumfanya awe kipenzi kikubwa kwa mashabiki wa pande zote mbili, Liverpool na Lile.
Awali origin alikanusha kujiunga na Liverpool mwezi Januari kupitia ukuraa wake wa mtandao wa Twitter, lakini tangu habari mpya izuke amekaa kimya kuhusu hilo.

0 comments :

 
Top