UKAWA YA PATA USHINDI WA BURE WA KIJIJI NA VITONGOJI VYAKE
Katika Wilaya Nachingwea CUF - Chama cha Wananchi kimezoa Kijiji kizima, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyambalapala na Wajumbe wake wote na Wenyeviti wa Vitongoji vya Nanjati na Mchangani.
Wagombea wa CCM wamerudisha fomu saa 10.15 alasiri zikiwa hazijaidhinishwa na Chama cha Siasa.
NAMTUMBO
Katika Kijiji cha Utwango, Kata ya Nabengo Wilaya ya Namtumbo, CUF imeshinda pingamizi dhidi ya mgombea wa CCM ambae aliwahi kutumikia kifungo ncha mwaka mmoja na miezi tisa mwaka 2009.
Hivyo CUF imeshinda bila ya Upinzani katika nafasi ya Mwenyekiti.
SONGEA
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimepita bila kupigwa katika mtaa 1 muhimu SONGEA mjini.
TABORA
Chama Cha Wananchi Cuf kimepata mitaa 3 Tabora mjini ikiwa ni pamoja na Kata yenye ushindani mkubwa ya kiloleni mtaa wa tabat baada ya mgombea wa CCM kushindwa kujitetea dhidi ya pingamizi alilo wekewa la kutokujaa kusoma na kuandika.
TANGA
Taarifa za mkoani TANGA CCM imepoteza vijiji na vitongoji 81 na kuna mapingamizi 233 mpaka sasa kwa vyovyote vile yanawatoa CCM kwenye ulingo.
Mhe Waziri mkuu ameingilia kati kuokoa CCM mkoani TANGA na kulazimisha wagombea wote waliotolewa wa CCM na wachache wa UKAWA waendelee na UCHAGUZI.
JIUNGE NA GROUP LA "UKAWA CANDIDATE 2015" UPATE HABARI SAHIHI ZA UCHAGUZI HUU.
STAY TUNE........
0 comments :
Post a Comment