
DARUSO umekuwa ni uongozi mbovu kupindukia kwa mwaka huu wa 2014-2015 hasa upande wa Serikali yaani kuanzia wizara zake zote
Bonanza lilikowa limeandalia na kampuni ya siomu za mkononi Airtel limevunjika leo siku ya jumamossi ambapo ilikuwa ni fainali za bonanza hilo.
Chanzo cha kuvunjika kwa bonanza hilo ambalo lilihusisha mchezo wa mpira wa miguu ni kile kilicho singiziwa kuwa ni kuepusha vurugu ambazo zinge ibuka endapo timu ya COSS (Courage Of Social Science) ingeibuka mshindi kutokana na mashabiki wa COET (Courage Of Engineering and Technology) kuonyesha kuwa na molali kubwa saana katika kushangilia.
Pambano hilo lilivurugika baada ya COSS na COET kutoka sare ya gori moja kwa moja hadi dakika ya tisini na hivyo kuamuliwa kupigwa penati.
Chanzo cha kuvuruga mechi hiyo isimalizike kwa kupigwa penati ni kushindwa kwa wizara ya michezo na wizara ya ulinzi DARUSO kushindwa kutoa msimamo wa mojaja kwa moja kwa kuwa wao walikuwa wanahusika katika kusimamia maslahi ya wanafunzi ambao wametumia mda wao mwingi kucheza mashindano yaliyokuwa ya wiki nzima, lakini pia kwa upande mwingine wao walikuwa na kzi ya kuhakikisha mashindano yanamalizika kama yalivyopangwa na kwa usalama.
Kwa mujibu wa wanafunzi mbali mbali ambao walikuwa wanashuhudia pambano hilo walisema kuwa kwa upande wao kama mashabiki hawakuona vurugu zozote zile ambazo zingeibuka, kwani kelele na mbwembwe za mashabiki ndizo zilikuwa zimetawala na zilikuwa za kiwango kidogo sana na ni kitu cha kawaida kwa mashabiki kushangilia na pia walikuwa wanashangilia kwa amani kabisa.
Wengi wao wameiangushia lawama wizara ya michezo na ulinzi kwa kushindwa kutoa maelekezo na msimamo wao juu ya shindano hilo na hasa kuonyesha kuwa hakuna vurugu zinazo weza kutokea kwa kuwa wanafunzi wametulia.
Kwa upande wao wizara ya ulinzi walionyesha mapungufu yao hasa pale walipokuwa wanajadiliana na baadhi ya wanafunzi waliokuwa wanalaumu kuwa hawajaona mchango wowote wa wizara hiyo kuhakikisha wanatoa upotoshaji uliokuwepo kuwa hakuna vurugu zingetokea endapo COSS wangeshinda.
Bonanza hilo lilishirikisha vitivo vyote 10 vya chuo kikuu cha Dar es salaam, SJMC, CONAS, UDBS, COHU, IKS, COICT, COET, UDSL, SOED na COSS. kati ya hivo ni vitivo vine ambavyo vilifanikiwa kuingia nusu fainali ambavyo ni UDBS, SOED, COET na COSS na kati ya hizo COET na COSS walifanikiwa kuingia fainali huku UDBS na SOED wakichuana kwa nafasi ya tatu na UDBS ikafanikiwa kumchapa SOED kwa penati.
Hii inaonyesha wazi ni jinsi gani DARUSO inaonyesha kufeli katika kuongoza serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam kwani kwa mwaka huu hii ni serikali mbovu ambayo haijawahi kutokea hasa upande wa mawaziri na uongozi wa juu yaani Rais na wenzie.
Kushindwa kumalizika kwa bonanza hilo ni dharau kubwa sana na aibu kubwa sana kwa wanafunzi wa UDSM ambao ni wanafunzi makini na wanaojua nini wanakifanya na si kama watu wanavyopotosha uma kwa kusema wataanzisha vurugu kisa ushindu wa kikombe cha Airtel. Haya ni maneno ya baadhi ya wanafunzi waliokuwepo uwanjani.
Wanafunzi walieleza kuwa kwa upande mwingine Airtel wameonyesha kuwa chanzo cha kukatishwa kwa bonanza hilo kwani walikuwa wakwanza kutoa sababu zisizo na msingi za kutoendelea kwa pambano hilo, na kinachoonekana ni hasira walizokuwanazo za kukataliwa kuleta wasanii na kuleta nyama choma ndani ya chuo hicho.
0 comments :
Post a Comment