TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Baada ya jana Kupigwa mabomu ya machozi wanachama wa CUF na mwenyekiti wake Mh.Ibrahim Lipumba,Hatimaye leo hii Mwenyekiti Mwenza wa chama kinachounda umoja wa wananchi (UKAWA) James Mbatia amechafua hali ya hewa Bungeni pamoja na wabunge wengine baada ya kuhoji juu ya Polisi kutumia nguvu na kumpiga Mh.Lipumba na wafuasi wake nini maana yake na Tafsiri halisi, kitendo ambacho kimekosa utatuzi kwa kutoelewana Bungeni,kufuatia Spika Makinda kuwataka wasubiri halafu wataona namna gani walijadili ,viongozi hao wametaka ufafanuzi huku wakihitaji majibu nahivyo wakihoji lini lipatiwe majibu kama alkivyosema spika wasubiri ndipo kukawa na mzozo Ulio mladhimu Spika Makinda Kuahirisha Bunge Hadi saakumi Jioni.
"Mbatia: Kujadili jambo la dharura kama kanuni inavyoniruhusu(Anazitaja kanuni husika). Mheshimwa spika jana tarehe 27 mwenyekiti wa chama cha CUF alikua na ratiba ya mkutano na maandamo yaliyoruhusiwa, cha kushangaza jeshi la polisi dakika za mwisho waliamuru yasitishwe, Lipumba alionyesha ushirikiano wa kusitisha lakini jeshi la polisi waliamua kutumia nguvu kwa wananchi waliokuwa wametulia ikiwemo kwa watoto wenye umri wa miaka mitano. Walisema wamepewa maagizo kutoka juu. 
Tunataka kujua hilo agizo kutoka juu limetoka kwa nani, tulijadili jambo hili kama ilivyo bunge ni cha kuisimamia na kuishauri serikali."alisema.
Source ITV

0 comments :

 
Top