TUME
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema inakusudia kuwafikisha Mahakamani
wananchi zaidi ya 100, wa Mkoa wa Njombe, baada ya kubainika kuwa
walijiandikisha zaidi ya mara moja kwenye daftari la kudumu la wapiga
kura.
Naibu katibu wa Tume hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Daftari na Tehama, Daktari, Sisi Kariali, ameiambia FikraPevu kwamba wananchi hao wamebainika kwa kutumia teknolojia inayotumiwa na tume hiyo na kwmaba zoezi hilo litaendelea katika maeneo yote nchini.
Aidha, amesema picha na majina ya watuhumiwa hao yamepelekwa kwenye idara zinazohusika huku akiwaonya wananchi ambao bado hawajaandikishwa kuacha kufikiria kwamba wanaweza kujiandikisha zaidi ya mara moja bila kubainika.
Amesema hadi sasa tume imekamilisha uandikishaji katika mikoa mitano (5), ambayo ni Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa na Njombe na kwamba hadi kufikia Juni 18, 2015, itakuwa imekamilisha uandikishaji kwenye mikoa mingine 8.
Kumekuwepo mjadala mkubwa baada ya kubainika kuwa watu wamekuwa wakijiandikisha zaidi ya mara moja katika vituo tofauti na kuibua hofu ya uchakachuaji mkubwa kufanyika katika Uchaguzi Mkuu 2015.
Katika hatua nyingine tume imesogeza mbele zoezi la kuandikisha wapiga kura kwenye mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga na Morogoro kutokana an mabadiliko ya mipaka ya yaliyofanywa na TAMISEMI.
Mikoa hiyo ambayo ilipaswa kuanza kuandikisha wapiga kura kuanzia leo, itaanza zoezi hilo ifikapo Juni 16, 2015.

Source Jamii Forum
0 comments :
Post a Comment