Mkurugenzi wa kampuni ya Lino International Agency, Hashimu Lundenga ametangaza kamati mpya ya maandaliza ya miss Tanzanaia baada ya kutoka kifungoni.
Kampuni hiyo imeamua kufanya mabadiliko ya kamati hiyo baada ya kuruhusiwa tena na BASATA kuendelea kuandaa mashindano ya miss Tanzania.
Mabadiliko hayo yamefanyika kwa kile walichokiita kuleta sura mpya ya mashindano ya miss Tanzania ili yaendane na usasa zaidi lakini pia ni watu kuchoshwa na kuziona sura zilezile kila siku katika maandalizi ya miss Tanzania.
Akiongea na waandishi wa habari Lundega, aliwataja wanaounda kamati hiyo kuwa ni Juma Pinto - Mwenyekiti wa kamati, Lucas Rutta - Naibu Mwenyekiti, Doris Mollel - Katibu na Jokate Mwegelo - Msemaji wa kamati hiyo.
Pia kamati hiyo itakuwa na wajumbe, Hoyce Tem, Mohamed Boazi, Glady Shao, Mgdallena Munis, Shaha Ramadhani, Ham Hashim, Khalfani Saleh pamoja na Ojambi Masaburi.
Kamati hiyo itakuwa na sekretariet ikiwa chini ya Dr. Ramesh Shah, Hidan Ricco, Yasson Mashaka pamoja na Deo Kapiteni.
Kwa mujibu wa Lundenga kamati hiyo itakuwa chini ya uangalizi wake kama mmiliki wa kampuni, kwani yeye hawezi kujitoa kabisa kwakuwa ni mmiliki wa kampuni hilo linalojihusisha na uaandaajai wa mashindano hayo.
"Kama nilivyo wahi kusema tangu awali kuwa wakati ukifika nitampa kijiti mwingine, na sasa wakati umefika. Sisi kama kampuni tumeteua kamati itakayokuwa inasimamia shughuli za shindano la miss Tanzania. Lakini hatuwaachi pekeyao, tuko nyuma yao ili tuwasaidie na sisi tunabaki kama wamiliki na waangalizi wa mashindano haya" alisema Lundenga
Pia aliwaasa wanakamati hao kwakuwa waadilifu kwani hakuna kitu kibaya kama kashifa katika mashindano. Aliwaeleza kuwa wasichana wanaokuja kwenyemashindano huwa tayari kufanya chochote kile ili washinde, hivyo wajiepushe na ushawishi huo na kuzingatia miiko ya mashindano.
Kwa upande wake Mwenyekiti mteule wa kamati hiyo Lucas Lutta, alisema kuwa kazi waliyonayo ni kuanza na changamoto zilizokuwepo ili kuzifanyia kazi na kuleta mvuto wa mashindano hayo kwakuja na mbinu mpya zaidi.
Pia msemaji wa kamati hiyo Jokate Mwegelo aliwashukuru BASATA kwa kuyaruhusus mashindano hayo na kutoa wito kwa mabinti waliokuwa wamekata tamaa na mashindano hayo, kutokana na kashifa zilizojitokeza, kuwa wawe tayari kujitokeza kwa wingi kushiriki na kuwa na imani na kamati hiyo kwani watakuwa katika mikono salama.
"Sisis kama kamati mpya tutafanya juu chini ili kuboresha mashindano hayo na kuyafanya kuwa ya kisasa zaidi na yaendane na hali halisi ya sasa" alisema Jokate
0 comments :
Post a Comment