Arusha.Diwani wa Chadema Kata ya Kiranyi
wilayani Arumeru mkoani Arusha,Patrick Bille ameeleza kwa masikitiko
jinsi bomu lilivyomlipua na kusema kwamba awali akiwa karibu na jukwaa
kuu aliona mfuko wa plastiki ukipepea angani ambao ulitua chini ya
jukwaa na kisha kulipuka.
Bille ambaye kwa sasa anaishi akiwa na vipande
vya chuma mwilini alisema kuwa,kabla ya mfuko huo kutua ardhini
alifikiri ni jiwe kwa kuwa alikuwa mita tatu tu kutoka ulipotua lakini
ghafla alishangaa kuona ukilipuka na kumjeruhi vibaya.
“Wakati nikiwa pale jukwaani niliona mfuko mweusi
ukipepea angani nikahisi ni jiwe limerushwa ghafla ulitua karibu na
nilipokuwa lakini nikasikia mlipuko ghafla na kuna vyuma vikanirukia
,”alisimulia Bille.
Hata hivyo,alisema kuwa hakumwona mtu aliyerusha
mfuko huo lakini ulitokea upande wa Baa ya Soweto iliyokuwa mkabala na
jukwaa kuu upande wa Magharibi.
Akiendelea kusimulia alisema kwamba mara baada
ya mfuko huo kulipuka alipigwa na vipande vya chuma katika eneo la kifua
chake na mkono wa kulia na kisha kupoteza fahamu na kujikuta akiwa
hospitali ya Selian.
Hata hivyo,alisema kuwa anakumbuka wakati akiwa
jukwaani kulikuwa na amani ya kutosha na neno la mwisho analolikumbuka
lilitamkwa na Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe ambapo aliwataka watu
wakichangie chama chao fedha za kuwawezesha kumaliza uchaguzi salama.
“Pale jukwaani nakumbuka kulikuwa na amani kabisa
lakini nakumbuka neno la mwisho alilosema mwenyekiti wangu kwamba watu
wachangie fedha za kukisaidia chama kishinde uchaguzi,”alisisitiza Bille
Diwani huyo kwa unyonge alisema kuwa baaya
kufikishwa hospitalini hapo madaktari walimwambia ya kwamba ameonekana
na vipande vya chuma mwilini ambavyo vimeingia umbali wa inchi mbili na
wanasubiria visogee ili viweze kutolewa.
1 comments :
kweli kunaumhimu wa kuwatambua viongozi wa dini kattika kuleta usuruhishi wa ugaidii....?
Post a Comment