TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

 




 Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ataongoza burudani katika shindano la kumsaka Redds Miss Mwanza linalotarajiwa kufanyika Juni 14, mwaka huu katika Viwanja vya Yatch Club jijini Mwanza.
Warembo 18 kutoka Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Mwanza wamejitokeza kushiriki shindano hilo.
Warembo wote wanatarajiwa kuanza kambi rasmi kesho Jumanne katika moja ya hoteli maarufu jijini humo.
Katika kumbukumbu la shindano la Miss Tanzania Mkoa wa Mwanza una historia za kutoa washindi akiwamo mrembo wa Tanzania, ambaye ni Nasreem Karim 2009 na Miriam Gerald 2010.
Pamoja na mchakato wa shindano la urembo kuendelea hivi sasa nchini, macho na masikio yapo mkoani Mwanza ambako kumekua kukileta changamoto na upinzani mkali kwa warembo kila mwaka.
Sugu atasindikizwa na mwanamuziki mwingine nguli kutoka katika Kundi la TMK ‘Wanaume Family,’ Juma Said maarufu kama Chege Chigunda

0 comments :

 
Top