
Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kesho inaanza kudhibiti namba za simu za mikononi mpya na zisizosajiliwa kwa kuzifungia. Pia imeishauri Serikali kuongeza kasi katika utoaji wa vishambulisho vya taifa ili viweze kutumika kuwatambua wahalifu .
Akizungumza jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa TCRA
Profesa John Nkoma alisema kuwa hatua hiyo imelenga katika kuhakikisha
kwamba inawadhibiti wateja wapya kutotumia namba hizo kabla ya
kujisajili.
“Kuanzia June Mosi mwaka huu (kesho),hakuna mtu
anayeweza kununua kadi ya namba za simu na kuitumia siku hiyo hiyo. Kuna
utaratibu maalumu umewekwa,.Pia kwa wateja wengine tumewapa nafasi ya
kuhakikisha wanajisajili na tumeongeza muda hadi Julai 10 wasipojisajili
tutawafungia rasmi,” alisema Profesa Nkomwa.
Akifafanua zaidi juu ya msimamo huo Profesa Nkoma
alisema ni kosa la jinai kutumia namba ya simu isiyosajiliwa na adhabu
yake ni faini ya Sh500,000 au kifungo cha miezi mitatu jela.
Akijibu lawama zinazoelekezwa kwa TCRA kwa
kushindwa kudhibiti matumizi ya simu kwa njia ya usajili, alisema
kumekuwa na tatizo linalotokana na baadhi ya wahalifu kugushi kwa
kuandika taarifa za uongo na picha zisizowahusu.
Alisema pia kuna haja ya watu kubadili tabia kwa
kuwaripoti watu wanaofanya matukio ya uhalifu yanayohusisha simu za
mkononi hasa wizi au lugha chafu, udanganyifu na usaliti.
“Simu naweza kuifananisha na kisu. Kinasaidia kama matumizi ni mazuri, lakini mhalifu anaweza kukitumia kudhuruo,”alisema Prof.
1 comments :
mbona wanatapatapa nao hawa, matra kuanzia leo hakuna kuruhusu simu zisizo sjiliwa, mara ohhh asiye sajiliwa kushughulikiwa kisheria. mbona hawana msimamo..? au ndo kuyaogopa makampuni ya simu.
Post a Comment