Leo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai wakati akitoa salamu za pole kufutia kifo cha Rais Magufuli, amewataka watanzania kuwa watulivu na kusema ilani ya CCM ya 2020 - 2025 na miradi yote ya maendeleo aliyoacha Rais Magufuli itatekelezwa kwani fedha zote za miradi hiyo zilikuwa zinapitishwa na Bunge.
Amewataka wabunge ambao kupitia kamati mbalimbali sasa hivi wako wanatembelea miradi hiyo kuwa watulivu.
SPIKA NDUGAI ameeleza kuwa " Ikumbukwe kwamba mheshimiwa Rais kwa nafasi yake ni sehemu ya pili ya Mhimili wa Bunge kwahiyo ni mdau wetu muhimu sana katika uendeshaji wa Bunge na shughuli za Bunge kwa ujumla wake kwahiyo tumepata pigo kubwa sana."
"Natoa pole nyingi kwa mheshimiwa makamu wa Rais, mama Samia Suluhu, viongozi wa serikali, kipekee tunatoa pole nyingi sana kwa mama Janeth Magufuli, familia ya mheshimiwa Rais wetu lakini kikubwa zaidi kwa watanzania wote popote pale walipo."
"Kama mnavyofahamu ndugu waandishi, waheshimiwa wabunge walikuwa katika ziara za kukagua miradi ya maendeleo kutokana na utekelezaji wa bajeti inayoendelea ambayo inaishia tarehe 30 June mwaka huu."
"Imebidi tutoe wito na maelekezo kwamba, sasa wabunge wote waliokuwa katika waliokuwa katika ziara hizo za ukaguzi wa maendeleo warudi Dodoma haraka sana. Kwahiyo wabunge wako njiani kutoka sehemu mbalimbali za nchi kurudi hapa Dodoma."
"Kama tunavyojua, mheshimiwa Magugufuli ana mambo ambayo alijipambanua mapema, ni mengi sana lakini kwa kifupi alikuwa ndio Rais mjenga nchi hasa katika eneo la miundombinu. Miundombinu ya barabara, reli, bandari, shirika letu la ndege, ujenzi wa viwanja vya ndege, miradi mikubwa mikubwa ya maji, miundombinu ya elimu, eneo la afya. Sijui ni eneo gani utaweza kusema kwamba mheshimiwa Rais ameweka kumbukumbu ya aina yake."
"Kwahiyo tunayo kazi kuwa sana sisi Watanzania ya kuhakikisha kwamba tunaendeleza nngwe ambayo amekwisha kuiweka ili kuhakikisha kwamba kazi zote alizokuwa akizisimamia ikiwemo ya utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-25 na kwa mambo mbalimbali ambayo aliyaainisha kupitia hotuba ambazo alizitoa hapa bungeni yeye mwenyewe tunaendelea kuzisimamia kwa faida kubwa zaidi ya Mtanzania."
0 comments :
Post a Comment