Taarifa zilizotufikia katika chumba cha habari zinaeleza kuwa wanafunzi wanne wa chuo kikuu cha Dar es salaam maarufu
kwa jina la Chuo cha Mlimani wamevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia
leo maeneo ya Yombo chuoni hapo. Wanafunzi hao wanaosemekana kuwa ni wa
mwaka wa nne na wa mwisho wa masomo walikuwa wanajisomea na kuandaa
“Disertation” zao na kujikuta wakivamiwa na watu wanne na kuamuriwa
watoe komputa zao na pochi za fedha. Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii
kutoka chuoni hapo, wanafunzi hao walikubali kuwapa komputa hizo na
pochi za fedha, na majambazi kuanza safari yao. Baadaye wanafunzi hao
wakawaomba wapate hata nakala (Soft Copy) ya vitu vyao, na ndipo mmoja
wao akaamua kuwafuata na kukumbana na risasi tumboni. Mwanafunzi huyo
baada ya kupigwa risasi alianguka chini na kugaagaa chini huku akikosa
msaada wa kupelekwa Hospitalini. Chanzo kimeendelea kusema kuwa
wanafunzi wa Chuo hicho waliwasiliana na uongozi ili kupata gari ili
wamkimbize mwenzao Hospitalini, lakini ilipita takribani nusu saa hakuna
majibu na ndipo walipoamua kujikusanya na kuamua kuwafuata viongozi.
Kwa sasa mwanafunzi huyo amekimbizwa Hospitalini kupata matibabu zaidi
na mpaka sasa hakuna taarifa yoyote iliyotoka, ingawa CHANZO CHETU
inajitahidi kufuatilia suala hilo ili kupta taarifa zaidi na picha za
tukio hilo. Tukio hilo limelaaniwa vikali na UMMA wa chuo kikuu cha Dar
es salaam na kuitaka serikali kufuatiliwa na kudhibiti vitendo hivyo vya
kikatili chuoni hapo. Endelea kufuatilia katika mtandao huu amboa
umefunga safari ya kuelekea Chuo kikuu cha Mlimani kuangalia nini
kinaendelea. Mbali na tukio hilo, pia kumekuwepo na wizi wa hadharani
katika shule za Chuo hicho ambapo hivi karibuni wanafunzi wamekuwa
wakiporwa komputa zao mchana kweupe maeneo ya Mikocheni wakitoke shule
kuu ya uandishi wa Habari na Mawasilinao ya Umma (SJMC). Suala hizi
limepoteza amani kwa wanafunzi na kuwafanya washindwe kusoma kwa amani
0 comments :
Post a Comment