TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Mchakato juu ya kodi mpya za laini za simu kulipiwa Tsh 1000 kila mwezi wananchi wengi wamesema hawajauelewa vizuri.

Tulipoongea na TCRA kupitia Msemaji wake Bw. Innocent Mungy, imesema haihusiki kabisa na kodi mpya za laini za simu.

Upande wa TRA imesema wao hawawezi kulitolea maelezo zaidi maana kazi yao ni kutekeleza maagizo wanayopewa na serikali.

Upande wa serikali kupitia wizara ya fedha imesema itatolea ufafanuzi hapo kesho kuhusu nani anapaswa kulipa hiyo kodi.

Naibu waziri wa fedha, Bi Janet Mbene amesema watafafanua kati ya mwananchi na makampuni ya simu nani anapaswa kulipa. Source EA radio

0 comments :

 
Top