
KESHO TAREHE (13/01/2014) NI MAPUMZIKO!
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ally Mohammed Shein kwa makubaliano na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete wametangaza kesho kuwa siku ya mapumziko ya kitaifa kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hayo yamesemwa na Dr. Shein katika hotuba yake ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi katika Uwanja wa Amani Zanzibar mchana huu.!
Chanzo EATV facebook page
0 comments :
Post a Comment