Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, alisema kuwa juzi walipata mapokezi makubwa mjini Kigoma na kwamba kila mtu akiwa katika chama afanye kazi ya kukijenga badala ya kukibomoa.
Alisema licha ya kuwapo na madai kuwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, ana umaarufu mkubwa mkoani humo, jambo hilo halina ukweli.
Alidai mwaka 2010 walitegemea kupata ushindi katika Jimbo la Mpanda, lakini Zitto aliandika barua akieleza kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, awe mgombea pekee.
Alisema baada ya chama kupata taaarifa na kutaka kumwajibisha Zitto, Mwenyekiti Mbowe, aliingilia kati na kusitisha uamuzi huo.
Alisema kutokana na waraka walioukamata aliodai uliokuwa na malengo ya kukisambaratisha chama, waliona hawana sababu za kuendelea na Zitto na kumvua nyadhifa zake na kwamba kitendo cha kuweka pingamizi mahakamani asijadiliwe kinamfanya awe mbunge wa Mahakama.
Alisema mwaka 2000 walikuwapo madiwani 11 katika jimbo la Zitto la Kigoma Kaskazini, lakini mwaka 2005 alipogombea walipungua na kubakia sita na kwamba mwaka 2010 walipungua zaidi na kubakia wawili, hivyo hakuna ukweli kuwa amekijenga chama katika jimbo lake.
Katika hatua nyingine na mwendelezo wa M4C OPD Umati mkubwa wa wakazi wa Manispaa ya Bukoba jana walimiminika kwa wingi katika uwanja wa Uhuru kuwasikiliza Viongozi wa Chadema waliohutubia mkutano wa hadhara.
Kabla ya mkutano huo, yalifanyika maandamano makubwa yaliyokuwa yakiongozwa na vijana waendesha pikipiki.Source: Nipashe Jumatatu.
Home
»
»Unlabelled
»
MAPOKEZI YA CHADEMA KIGOMA YAMSHANGAZA LEMA
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
1 comments :
tunawatakia kila la heli CHADEMA
Post a Comment