TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749



Mwenyekiti  wa kamati ya  hamasa  mkoa wa Iringa Selina Charlesy Kisyeri  akiwahutubia  wakazi wa jimbo la Iringa mjini ktk uwanja wa Mwembetogwa leo

Wananchi  wakifuatilia mkutano  wa Chadema leo

Iringa  wakifurahia majibu ya Chadema dhidi ya CCM jimbo la Iringa mjini

 
mwenyekiti wa kamati ya hamasa kanda ya kusini John mwambigija  akijibu mapigo ya naibu katibu mkuu wa CCM Bara Mwigulu Nchemba ya  kudai ataopngoza mapambano kumtoa mbunge Peter Msigwa  mwaka 2015  huku kada huyo wa Chadema  akidai kama  waziri mkuu wa Mbeya Rais wake Sugu  wataongoza mapambano kuhakikisha CCM haimtoi Msigwa 

Mwenyekiti  huyo ametoa kauli hiyo  leo  wakatio akiwahutubia  wananchi wa jimbo la Iringa mjini katika  uwanja wa Mwembetogwa  ikiwa ni  siku mbili toka Nchemba kutangaza mikakati ya CCM katika kumwondoa mbunge Msigwa.

Alisema  kuwa kutokana na kazi mbali mbali za kimaendeleo alizozifanya mbunge Msigwa katika jimbo  hilo ni vigumu kwa CCM kuchukua jimbo hilo na kuwa atakuwa  wa kwanza  kuongoza mapambano ya kutetea  jimbo hilo.

Alitaja  baadhi ya kazi  zilizofanywa na mbunge Msigwa kuwa ni pamoja na kupeleka  vitanda  Hospitali ya  wilaya ya Frelimo,madawati mashuleni ,kuanzisha  ujenzi wa shule ya  sekondari Nduli na kuwa fedha  mamilioni zaidi ya 20 ya mfuko wa jimbo  zimepelekwa  huko.
 
Wakati  huo huo  jeshi la polisi  limewataka  viongozi wa Chadema mkoa wa Iringa  kesho asubuhi na mapema  kufika ofisi za  jeshi  hilo wilaya ya Iringa mjini kutokana na kuzidisha muda wa mkutano badalay ya kumaliza saa 12 kamili wamemaliza saa 12.7 jioni.         

0 comments :

 
Top