TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


Tasisi kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Kilimanjaro, imewatia mbaroni wafakazi  watatu na kuwachunguza wawili wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco),  kwa kosa kuomba na kupokea rushwa ya Sh. 400,000.

Wafanyakazi hao wanadaiwa kwenda nyumbani kwa Baltaza Zafa Ally, mkazi wa Shant Town Manispaa ya Moshi, kwa malengo la kukata umeme wa nyumba hiyo kwa madai kuwa alikuwa akidaiwa na shirika hilo.

Baada ya akufika nyumbani kwa mteja huyo walikuta geti limefungwa ndipo walipoingia kwa kuruka ukuta wa geti na kuanza kukagua mita ya umeme na kudai kuwa mita hiyo imechezewa na kumtaka mteja huyo awalipwe Sh. million moja ili wasikate umeme.
Baltaza aliiambia NIPASHE kuwa, watuhumiwa hao walifika nyumbani kwake kwa kuruka ukuta na kuingia ndani na kuanza kusoma mita, baada ya kumaliza kusoma miti hiyo ndipo walipomwambia kuwa mita hiyo imeonekana kuchezewa na kisha kumwambia awape fedha ili wasikate umeme.
“Mimi nilitoka ndani na kuwakuta wakiwa kwenye mita yangu na hii ni mara ya pili kufika nyumbani kwangu,” alisema.

Alidai kuwa mara ya kwanza watuhumiwa hao walifika na kusoma mita hiyo na kumwambia kuwa mita hiyo inaonyesha kuwa imechezewa na kudai walipwe Sh. 500,000 kwa madi kuwa ili wasitoe taarifa kwenye shirika hilo.

Alisema Mei 31, wafanyakazi hao walirudi ten, na kukuta geti likiwa limefungwa ndipo waliporuka ukuta na kuingia ndani na kusoma mita na kudai imechezewa na kutaka wapewe Sh. 1000,000 ili wasikate umeme huo.

Alisema baada ya kutakiwa kutoa fedha hizo fedha aliwaeleza kuwa hana, walikata umeme.

“Kwali baada ya kuniomba Shilingi milioni moja, mimi niliwaambai kuwa sina fedha hiyo, ndipo walipokata umeme huyo lakini cha kushangaza bado walikuwa wakiendelea kunitaka niwape pesa ili waurudishie umeme huo, na mimi nilichowaambia pesa niliyonayo ni Sh. 400,000, na kuomba niwape hiyo na kiasi kilichobaki watakuja kukichukua na ndipo waliporudisha umeme,” alisema

Aliongeza kuwa aliamua kwenda Takukuru ili kutoa taarifa hizo.

Meneja wa Tanesco mkoa wa  Kilimanjaro, Martin Kasyanju, alithibitisha kukamatwa kwa wafanyakazi wake, na kusema kuwa wafanyakazi watatu walikamatwa na Takukuru, kwa kupokea rushwa huku wengine wawili wakiwa katika  uchunguzi.

Alisema kuwa kumekuwapo na malalamiko ya muda mrefu kwa wafanyakazi hao na kwamba hatua ya kwanza ambayo  ameichukua ni kuwaachisha kazi ili sheria ichukue mkondo wake

Kasyanju alisema aliwakabidhi wafanyakazi hao kwa kamanda wa Takukuru ili awafungulie mashtaka na kwa taarifa alizonazo ni kuwa leo.
Hata hivyo jitihada za kumpata Kamanda wa Takukuru wa Mkoa wa Kilimanjaro, Lawrence Swemu, kuthibitishatukio hilo hazikufanikiwa baada ya simu yake ya mkononi kutopatikana na hata mwandishi alipokwenda ofisini kwake alijibiwa kuwa alitoka nje ya ofisi.
CHANZO: NIPASHE

0 comments :

 
Top