TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Jeshi la polisi zanzibar limefanikiwa kumkamata mtu mmoja akiwa na mabomu manne ya kivita ambayo yanasadikiwa ni miongoni mwa mabomu yanayotumika katika vitendo vya uhalifu yaliyotokea sehemu mbali mbali nchini.
Kamishna wa jeshi la polisi zanzibar CP Hamdani Omar Makame amethibitisha kukamtwa kwa mtu huyo ambaye kwa Mujibu wa jeshi hilo mtu huyo amekiri kuwa anajishughulisha na mtandao wa kuagiza, kuingiza na kuhifadhi mabomu yakivita ya kurushwa kwa mkono na mabomu hayo yalikuwa matano na polisi wamesema huenda moja ya hilo likawa ndilo lilotumika Darajani huku kamishna amemsmea mtandao huo unausihwa na matukio kadhaa.

Hata hivyo kamishna Hamdani Maka amesema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye hatahivyo amekataa kumtaja jina na mazingira yaukamataji wake amemsemea hahusiani na imani ya kidini na polis inamshughulika mtu kisheria kutokana na kosa lake kwa mujibu wa sheria za nchi nasiyo Imani za kidini.
Wakati polis imekataa kutoa taarifa yeyeote kuhusu mtuhumiwa huyo jeshi hilo limesema hakuna kosa lolote la kisheria endapo mtu akipelekwa nje ya zanzibar kwakosa la ugaidi huku akisema bado polisi inaedelea na upelelezi wa tukio hilo kama ni la zanazibar au la, ama ni mtandao waugaidi wa nchi nzima.

0 comments :

 
Top