TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Ndungu zangu UKAWA siku wanatoka bungeni Yalisemwa mengi mpaka kuiita ni intarahamwe wengine wanataka kuongea kwa kwa kutumia sehemu zingine za kuongelea kama zingeweza kuongea, ili waonekane wapo na wanatetea msimamo wa chama chao ili wasifukuzwe kama ilivyo agizwa na viongozi wao. 
Wengi wana CCM walitoa kauli za kejeli na za kuudhi kwa wenzao, kwakuwa tu  UKAWA wanatetea mapendekezo ya wananchi na si mapendekezo yao wenyewe.


Hizi ni baadhi ya kauli zao wana CCM walizokuwa wakizitoa kwa UKAWA...........................................

NAIBU SPIKA; hebu hesabu mistari kama imetimia tunaendelea na kikao, hawatutishi wachache tu" 
WASIRA; wanafikiri wataitwa ikulu wakanywe chai, hiyo hakuna.
MWIGURU; "hawapati posho hapa wakajambie mbele huko na ushoga wao"
LUSINDE; tutaendelea hivi hivi na katiba itapita..
KOMBA ( Analia) "nasema hivi katiba serikali 3 ikipita naingia Mstuni"
NAPE; Wakiingia kwa wananchi, nasi tutazunguka nchi nzima, 
Hizo ni baadhi tu ya pumba zilizosemwa na hao............................. 

Kutokana na msimamo wa UKAWA na umhimu wao katika kufanikisha upatikanaji wa katiba, sasa viongozi haohao wana CCM wamegeuka na kuona kuwa UKAWA wanapaswa kurudi Bungeni kwa kuwa wao ni muhim saana juu ya upatikanaji wa katiba mpya.


kila kiongozi toka CCM amekuwa akitoa ombi lake kwa UKAWA kurudi Bungeni ili mchakato wa kuipata katiba mpya uendelee, na hakuna tena ambaye anawakejeli na kuwatolea maneno ya kashifa na dharau UKAWA.


Na hizi ni baadhi ya kauli za viongozi wa CCM kwa UKAWA kwa sasa.

JK akiwa Mbeya; "UKAWA Wananiweka njia panda bila wao katiba haipatikani"
PINDA akiwa Tanga "Ukawa ni muhimu sana ktk Upatikanaji wa katiba..
SITA; "Tutawaita UKAWA kwenye Meza ya Mazungumzo yaishe......
MSAJILI ; "Nitaviita vyama vyote ili Tuyamalize......

Hii inajionesha wazi kuwa viongozi wengu toka CCM huwa hawawezi kufikilia ni nini madhara ya kupuuzia maoni ya wananchi na hivyo kwakuwa wanaamini wao wanamashabiki na wanachama wengi kila kitu kitapita na kushinda kwa kishindo. Wanasahau kuwa Wananchi wanauelewa mkubwa kwa sasa juu ya umhimu wa katiba yenye mabadiliko na sio yenye ubabe mkubwa kwa wananchi na kuwalegezea baadhi ya viongozi wa juu pale wanapofanya maovu.


Watanzania mjue kuwa UKAWA hakuna jambo ambalo limetoka katika mapendekezo yao ambalo wanalisimamia, bali wansimamia na kutetea maoni ya Wananchi yaliyo katika rasimu ya katiba, ambayo yalikusanywa na tume ya katiba iliyokuwa na wataalamu ya nyanja mbalimbali na siwanasiasa ambao wao wanaangalia ni njia gani itawaletea urahisi katika kupata vyeo na kushinda majimboni kwao.



WATANZANIA TUAMKE, TUJITAMBUE, UKAWA NI KWA AJILI YETU NA MAONI YETU. juu ya katiba mpya ambayo ni yetu na vizazi vingine vijavyo. wanaotaka kuweka maoni yao mjue kuwa wao wanauhakika na vizazi vyao, kwakuwa wamesha vitengenezea njia na wanataka wazidi uvitengenezea njia ya kuendelea kushika atamu na kuishi maisha mazuri.

UKAWA endeleeni na msimao wenu kwani inaonyesha kuwa serikali iliyopo haikujipanga kuleta katiba mpya, bali kuleta katiba ya kwao wenyewe. Ninaimani Watanzania wako pamoja nanyi........

0 comments :

 
Top