
Siku ya tarehe 19 Juma tatu ilikuwa ni siku ya kikao cha dharula kwa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam, (DARUSO) abapo ajenda kuu ilikuwa ni kujadili maendeleo ya DARUSO ikiwa imewasilishwa na Rais wa DARUSO Nickson Filbert.
Hoja hiyo ilizua vutano baina ya wabunge na kiti cha spika kwa kuwa wabunge walikuwa wanahoji uhalali wa udharula wa kikao hicho kwakuwa ajenda haifanani na udharula kama ilivyokuwa ietangazwa na spika wa bunge.
hata hivyo kutokana na ubabe wa pika wa bunge aliokuwa anauendsha ndani ya kikao hicho alilazimisha wabunge kutoendelea na kuomba muongozo juu ya jambo hilo. mmoja ya wabunge hao Mh Ipyana ni kati ya wabunge waliokuwa wanahoji uhalali wa kikao hicho na kutaka kujua kama kunamajina ya wabunge waliosaini ili kukipa uhalali wa kikao hicho.
Lakini kwa sauti ya ukali na ya kibabe pika wa bunge alimuaulu mbunge huyo kukaa chini.
"Mheshimiwa Ipyana onyo la mwisho na hivyo kaa chini" alisea, na hivyo Ipyana alikaa chini na hivyo Rais wa DARUSO kuendelea na kutoa hotuba aliyokua ameandaa.
Katika hotuuba yake alisema kuwa kunamambo makuu matatu ambayo ndiyo sababu ya kikao hicho, na mambo hayo ni:-
1-Kutoa ufafanuzi kwa mambo yasiyo sahihi
2-mabadiiko ya baraza la mawaziri
3-kuangalia cha kufanya ili kuzidi kusonga mbele.
Akizungumzika juu ya mambo ambayo hayako sahihi kama watu wanavyoamini na kusikia alisema kuwa, kumekuwa na mgogoro baina ya mawaziri, wabunge na mahakama kutokana na idadi ya viongozi watakaobaki ili kuwasaidia wanafunzi wanaokuwa maeneo yao ya kufanyia field/mafunzo kwa vitendo, kwa ni bunge lilipitisha kubaki watu watatu yani Mwenyekiti, Katibu, na Excom Accademic lakini kutokana na msimamo wa Rais wa DARUSO alikataa idadi hiyo na kutaka kubaki mtu mmoja tu kitu ambacho kilipingwa vikali na wabunge, makatibu na wenyeviti wa vitivo mbalimbali.
Alieleza kwa kujitetea kuwa utata huo ulisababishwa na utawala kukataa kutoa pesa zilizokuwa zinatakiwa kuwapa viongozi watakao baki kama posho ya chakula na malazi. kitu ambacho kisingizio tangia mgogoro huo umeanza.
Akiongelea suala la mabadiliko ya baraza la mawaziri, alisma kuwa, hakuna aliyemwondoa madarakani kwa sababu ya siaa bali ni kutokana na utendaji wake wa kazi mbovu aliouonyesha kwa kipindi chote hiki cha rikizo.
Pia aliongza kwa kusema kuwa uteuzi huo umefanyik kwa kizingatia ushauri kutoka ofisi mbalimbali ikiwemo ofisi uya mshauri wa wanafunzi.
Alifafanua kuwa uteuzi kwa mawaziri ni upendeleo tu kwa hiyo wale ambao walikuwa wamechaguliwa ilikuwa ni upendeleo kwao na wanaoteuliwa tena pia kwao ni upendeleo tu.
Mawaziri walioteuliwa katika nafasi mpy za uwaziri zilizokuwa zimeachwa wazi ni:-
-Gipson George-amepewa nafasi ya uwaziri mkuu
-Mboya Inocent- amepewa nafasi ya unaibu waziri wa ulinzi
-Emoneza Emmanuel- nafasi ya uwaziri wa cafeteria
-John Fabian- aliyepewa nafasi ya uchief protocol.
0 comments :
Post a Comment