Zitto Kabwe awabeza UKAWA na kuwaita "Wasaka Tonge tu"
WanaJamvi:
Mh. Zitto Kabwe, leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa instagram #zittokabwe amewakebehi viongozi wa UKAWA.na kuwaita ni wasaka tonge tu.
Huku akiwa ameposti picha ya gazeti la Mtanzania lenye kichwa cha habari " UKAWA Wapanga safu yao"
Hapa nanukuu maneno yake neno kwa neno anasema:mwisho wa kunukuu."Taifa limevimba. Wakulima Mahindi yanawaozea na Mpunga bei imeporomoka sababu ya mchele kutoka nje usiolipiwa kodi. Wahisani wamezuia misaada (sababu ya kashfa ya #tegetaescrow ) kiasi serikali haiwezi kujiendesha.
Unapoona wanasiasa wanagawana vyeo katika nyakati kama hizi, ujue Taifa halina Viongozi bali wasaka utawala.
Wasaka utawala baada ya uongozi ni #wasakatonge tu"
Katika ukarasa wake huo kuna wachangiaji mpaka sasa zaidi ya 140, walio wengi wamekuwa wakimponda kwa hatua yake ya kuwashambulia UKAWA.
My Take:
Inakuwaje Mh.Zitto anawaponda na kuwakebehe UKAWA ambao wamesaini makubaliano hivi punde?
Je! Bwana Zitto kajitoa rasm upinzani?
Source : Instagram: Zittokabwe
0 comments :
Post a Comment