TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Jumapili iliyopita nilikuwa napita mitaa flani ya posta mara nikawaona wazungu wakitoka hotelin wakapanda gari wakaondoka zao kucheki pale chini lilikopaki lile gari ya wale watasha nikaona waleti nikaifata nikaokota hakuna mtu aliyeniona nikasepa zangu mpaka home. 

Kufika home nikaifungua nikakuta kuna dollar za kimarekani 1500 na zetu za madafu kama 50,000 hivi, pia nikaona hati ya kusafiria pamoja na contact mbali mbali za mhusika. Ki ukwel nilikuwa sina pesa cku ile lkn nikaingiwa na huruma kwa muhusika jinsi atakavyoangaika kutafuta,nikaamua kufunga safari kurudi kule hotelini kumtafuta mhusika nimkabidhi vitu vyake,kufika pale kwel nilikuta wamerudi nikamuita mmoja wao ambaye ndio alikuwa ndie haswa mhusika wa vile vitu nikamkabidhi akashangaa sana ikabidi anipe noti 5 za elfu kumi kwa ajili ya asante nikajifanya kukataa kiaina mwisho wa siku akanipa contact zake nikasepa.

Baada ya mwezi mmoja kupita mara cm yangu ikaita kupokea naambiwa njoo serena hoteli tuonane kufika pale nikakutana na yule mzungu akanambia nimekuletea zawadi yako kwa sababu nimeona wewe ni kijana mzuri mana tumezoea watanzania wengi ni watu wenye tamaa sana. Kwa hiyo nimekununulia gari range lover vogue na kiasi cha pesa zaidi ya bilioni kumi ili ufanye biashara.

Mara nikasikia kaka chakula tayali huku amka tule......du kumbe nilikuwa naota tena mchana kweupee.

0 comments :

 
Top