Mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA leo walikuwa na mkakati wa kuendesha mafunzo kwa viongozi wa chuo kikuu cha Dar es salaam kuhusu jinsi ya kujaza fomu za kujiandikisha vitambulisho vya taifa kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam.
kazi hiyo iliingia dosari baada ya viongozi mbalimbali wa serikali hiyo ya wanafunzi kuanza kuhoji utaratibu wa kuendesha mafunzo hayo kwani kulikuwa hakuna taarifa yoyote ile iliyokuwa inaeleweka kuhusu jinsi gani mafunzo yataendeshwa na yatandeshwa kwa malipo au hakuna malipo.
Baada ya kuuliza maswali hayo ndipo uongozi wa ngazi ya juu wa serikali ya wanafunzi wa DARUSO chuo kikuu cha Dar es salaam, ukaamua kutoa maelezo kwakuanza na Chief Protocol ambaye alisema kuwa uataratibu ulishatolewa mapema kuwa mafunzo hayo yatatolewa bure na viongozi hao watafanya zoezi la kugawa fomu na kutoa elimu kwa wanafunzi wengine kwa wiki mbili bure pasipo malipo yoyote yale iosipokuwa waliiomba mamlaka ya vitambulisho kutoa vyeti kwa viongozi hao.
Maelezo hayo toka kwa Chief Protocal yalichafua hali ya hewa kwa viongozi wengine kwani moja kwa moja alionekana kuwa upande wa NIDA na kuonyesha kunanamna ambayo yeye kama kiongozi wa juu na viongozi wengine wa juu wamewezeshwa na NIDA ili kuwarubuni viongozi wengine kwa kuwashawishi wafanye kazi ya kujitolea huku wao na NIDA wakunufaika.
Kila kiongozi alinyenyua mkono kutaka kuongea na kutoa ufafanuzi juu ya jambo hilo, na walipo pewa nafasi ya kuongea wengi wao walianza kwa kuulaumu uongozi wa serikali ya DARUSO kwa kutotoa taarifa iliyokamilika huku wakiahidi kwa NIDA kuwa taarifa zimeeeleweka kwa viongozi wote. Pia walihoji kwa upande wa NIDA kama wao hawajapewa fedha na serikali kwaajili ya kuendeshea zoezi hilo.
Msemaji wa NIDA kwa waliokuja kutoa mafunzo hayo, alisema kuwa NIDA haijapewa pesa kwa watendaji wa kazi hiyo isipokuwa imepewa pesa ya vifaa vya kuwezesha kazi hiyo. Majibu hayo yaliwakela wanafunzi hao kwa kuona wanakejeliwa na wanadhalauliwa kwa kufanywa watoto huku wakiwa wanatambua kuwa NIDA imepewa pesa za kutosha za kuwezesha zoezi hilo inchi nzima.
Kutokana na mvutano huo viongozi wa DARUSO waliona kabisa kunanjama za NIDA kutaka kuwatumia wanafunzi kufanya kazi ya kujitolea huku wao wakiweka pesa mifukoni mwao ambazo zilitakiwa kifanyia zoezi hilo.
Mvutano huo ulimfanya makamu wa Rais wa serikali ya DARUSO UDSM kusima na kutaka kuwashawishi viongozi wenzake kutulia na kuruhusu mchakato uendelee kwa mfumo huohuo wa kujitolea huku akitumia maneno ya kuwashawishi zaidi lakini kutoakana na ukomavu wa viongozi hao bado wakampinga na yeye pia na kumuona naye ni kati ya viongozi wanaotaka kuwarubuni viongozi wenzao.
Mrumbano hayo yalimfanya waziri mkuu wa DARUSO, Gibson, kuja kutoa ufafanuzi ambaye alisema kuwa hata wao walipokaa na NIDA kujadili jinsi ya kufanikisha zoezi hilo, waliwaambia kuwa, kufanya kazi hiyo bure wanauhakika viongozi wengi watapinga kutokana na ugumu wa kazi yenyewe lakini na majukumu mengi waliyonayo na ukubwa wa mamlaka hiyo"NIDA". Ndipo akatoa kauli ya kusitisha mafunzo hayo hadi pale NIDA watakapo kuja na njia nyingine tena kitendo ambacho kiliungwa na viongozi wote na kuahirisha mafunzo.
Zoezi la kuandikisha wananchi ili wapate vitambulisho vya taifa limekuwa likiendelea sehemu mbalimbali nchi nzima huku ikionekana ni changamoto kwa wanafunzi hasa wanavyuo ambao mda mwingi huwa vyuoni na kulikosa zoezi hilo pale llinapoendelea makwao kitendo ambacho kiliibua hii njia ya kuwaandikisha wakiwa vyuoni kwao.
0 comments :
Post a Comment