TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

  
Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU Mhe Rweyemamu atajwa katika KASHFA nzito ya Matumizi makubwa ya fedha za UMMA ili kuipigia UPATU Katiba pendekezwa ipigiwe KURA ya "Ndio".

Mpango huo uliopewa jina la" Media Plan" wenye lengo la kuipigia chepuo Katiba pendekezwa ipigiwe kura ya NDIO kwa kuanzia unalenga kuvishika vituo vya Televisheni 7. ambapo vitakuwa vikitoa matangazo mfurulizo kwa siku 22..
Katika matangazo hayo kuna orodha ya wasomi 20 watakaokuwa wakipishana kuwashawishi watanzania kupiga kura ya NDIO kwa siku 22 mfurulizo kwenye vituo hivyo vya Televisheni.
Katika mkakati huo kunawatangazaji wa Televisheni 9 watalipwa mamilio
ni ya pesa kwajili ya kuanda vipindi vutakavyo kuwa vikipigia DEBE Katiba pendekezwa ipigiwe kura ya NDIO.
Mkakati umevitaja vituo 22 vya REDIO nchini kufanya kazi mfurulizo kuwa shawishi watu kupiga kura ya NDIO huku wakitafutwa watu wenye malengo yanayofanana na kura ya NDIO kuwahoji ili kufanikisha kuhadaa UMMA.
.Mkakati unaeleza kuwa Magazeti yote yanayomilikiwa na watu binafsi isipokuwa magazeti ya Cuf na Chadema yatapatiwa fungu maalumu la fedha kwajili ya kuipigia DEBE katiba pendekizwa kwa siku 22 mfurulizo.ikiwa ni pamoja na kuwahoji watu wa NDIOOOO tu
Mkakati pia unaeleza kuwa wahariri wote watalipwa mamilioni ya fedha kwajili ya kuhakikisha wanainajisi taaruma yao na kuipigia DEBE katiba pendekezwa kwa kuwahimiza wananchi kupiga kura ya NDIO
KAULI YA IKULU:
Akuzungumzia tuhuma hizo, Mkurugenzi wa mawasiliano IKULU Bwana Rweyemamu alisema -"Kwani kunaubaya gani , Kama wao wana kwenda kuwambia watu wapige kura ya HAPANA wajue kunaupande mwingine watapita waseme pigeni kura ya NDIO na ndio tunavyofanya sisi.
SWALI LANGU
Huu upande wa NDIO unatumia pesa zetu wote Je ule wa HAPANA utatumia pesa zipi wakati wote tunakamuliwa kodi na wote tunakai ya kuamua NDIO au HAPANA...?
By  Bakari Nzimano

0 comments :

 
Top