Raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, Dokta Ali Mohamed Shein amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuacha kutumia vibaya mchakato wa Katiba Inayopendekezwa kwa lengo ya kuwagawa wananchi na kutishia amani na utulivu uliopo nchini.
Shein aliyasema hayo jana katika ukumbi wa Grand Palace, Zanzibar wakati akizungumza na wananchi na viongozi wa CCM katika maadhimisho ya miaka minne ya kuwepo madarakani tangu aliposhinda Urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.
Pia ameelezea kukerwa na kuchoshwa na matusi yanayojitokeza katika kipindi hiki kutoka kwa baadhi ya viongozi, huku akisemaRais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuacha kutumia vibaya mchakato wa Katiba Inayopendekezwa kwa lengo ya kuwagawa wananchi na kutishia amani na utulivu uliopo nchini.
“Nitawachukulia hatua za kisheria na kinidhamu viongozi wanaotumia vibaya mchakato wa kupata Katiba mpya kwa kutoa kauli za chuki na kutukanana katika majukwaa… nitatumia Katiba na Sheria na sio ubabe kwa sababu sio kawaida yangu kufanya hivyo,” alisema.

Alisema kumeanza kujitokeza viashiria vya kuanza kuvuruga amani na utulivu iliyopo sasa kwa kisingizio cha mchakato wa rasimu ya Katiba Inayopendekezwa hivi sasa.
Alisema Katiba Inayopendekezwa ni mkombozi kwa wananchi wa Zanzibar kwa sababu imejibu hoja za malalamiko na kero za Muungano ambazo awali zilikuwa zikilalamikiwa na wananchi ikiwemo wanasiasa.
Akifafanua, alisema kwa muda mrefu wananchi wa Zanzibar walikuwa na malalamiko mengi katika Muungano ambayo kwa bahati nzuri katika Katiba Inayopendekezwa yamepatiwa jawabu sahihi.
Kwa mfano alisema si kweli kwamba Muungano uliopo sasa umeimeza Zanzibar na haitambuliwi katika jumuiya za kimataifa.
Ameelezea kushangazwa na tabia ya vyama vya upinzani kususia mchakato wa Katiba wakati ndio waliokuwa mstari wa mbele kulilia uwepo wa Katiba mpya.
Aidha, ameelezea kushangazwa na msimamo wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuikataa Katiba Inayopendekezwa, ilhali mambo anayoyalilia yamo katika katiba hiyo.
Alisema Katiba Inayopendekezwa imetoa fursa kubwa kwa Zanzibar kufanya mambo yao kwa mapana zaidi ikiwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema Katiba Inayopendekezwa ni kwa maslahi ya Watanzania ambayo imezingatia mambo yote muhimu ikiwemo kwa upande wa Zanzibar.
Alisema: “Nimesikitishwa sana mwenzangu, Makamu wangu wa Kwanza wa Rais amekuwa akisisitiza kutungwa kwa sera za nishati na mafuta kwa ajili ya kujitayarisha kuchimba mafuta, lakini yeye Katiba Inayopendekezwa haikubali.”
Akifafanua zaidi alisema Baraza la Wawakilishi ndiyo lililopitisha azimio la kutaka nishati ya mafuta na gesi kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano. Aidha, alimtaka Maalim Seif kuacha kuwashawishi wananchi wa Zanzibar kuikataa Katiba Inayopendekezwa akisema yeye sio msemaji wa wananchi wa Zanzibar.
“Msemaji wa wananchi wa Zanzibar wote ni mimi na sio yeye…nawataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya kuipitisha Katiba mpya Inayopendekezwa,” alisema.
Dokta Ali Mohammed Shein
Alisema Katiba Inayopendekezwa imezingatia mambo yote ambayo wananchi wa Zanzibar wametaka kuzingatiwa na kusisitizwa ikiwemo mafuta na gesi.
Alisisitiza na kusema Katiba Inayopendekezwa imezingatia na kuuenzi Muungano wa Tanganyika wa Zanzibar pamoja na Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ambayo yameasisiwa na viongozi wakuu wa nchi mbili hizo.
Aidha, Dk Shein amesema amekubaliana na kuridhishwa na Katiba Inayopendekezwa ambayo imetoa kipaumbele kwa Zanzibar kupiga hatua kubwa ya maendeleo.
Alisema mambo yaliyobakia katika Muungano ni muhimu sana ikiwemo ulinzi na mambo ya elimu ya juu ambayo yatasaidia kuwawezesha vijana kupata elimu ya juu kwa kutumia bodi mbili za elimu.
========================================================================
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akizungumza na Wananchi wa CCM na Wanachama katika Kongamano maalum la maadhimisho ya sherehe za miaka minne ya Ushindi wa CCM na kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Grand Palace Mjini Zanzibar.
Baadhi ya wanachama wa CCM walioshiriki katika Kongamano maalum kwa ajili ya kusherehekea miaka minne ya ushindi wa Dk.Ali Mohamed Shein kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baaraza la Mapinduzi wakimsikiliza Makamo Mwenyekiti wa CCM alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Grand Palace Mjini Zanzibar
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na baadhi ya Viongozi wa Chama baada ya kulifungua Kongamano la CCM katika kusherehekea miaka minne ya ushindi wa CCM na Dk.Ali Mohamed Shein kuwa Rais wa Zanzibar lililofanyika katika ukumbi wa Grand Palace Mjini Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa Kamati Kuu Ya CCM Balozi Seif Ali Iddi katika Hoteli ya Grand Palace Mjini Zanzibar baada ya kulifungua Kongamano la CCM katika kusherehekea miaka minne ya ushindi wa CCM na Dk.Ali Mohamed Shein kuwa Rais wa Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai katika Hoteli ya Grand Palace Mjini Zanzibar baada ya kulifungua Kongamano la CCM katika kusherehekea miaka minne ya ushindi wa CCM na Dk.Ali Mohamed Shein kuwa Rais wa Zanzibar
CHANZO: JAMII FORUM
0 comments :
Post a Comment