TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

                           
London. England. Mashindano ya urembo ya dunia yamemalizika jana huku mrembo kutoka Afrika Kusini, Rolene Strauss akiibuka Miss World 2014 katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa ExCeL London jijini London, England.
Nafasi ya pili ilikwenda kwa mrembo wa Hungary, Edina Kulcsar huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na mrembo wa Marekani, Elizabeth Safrit.
Warembo walioingia katika hatua ya tano bora ni kutoka katika nchi za Hungary, Australia, Marekani England na Afrika Kusini.
Kwa mwaka huu Afrika ilifanya vema baada ya mrembo kutoka Kenya kutinga katika hatua ya 10 bora pamoja na mrembo wa Afrikia Kusini.
Walioingia hatua hiyo ni Australia Mexico, Marekani, Kenya, Hungary, Brazil, Guyana, England, Afrika Kusini na India.
Kabla ya yote walitangazwa warembo walioingia 25 bora kupitia nchi zao;
Bolivia, China , Brazil, Jamhuri ya Dominican, England, Mexico, Guyana, Hungary, India, Indonesia, Malaysia, Sudan Kusini, Vietnam, Finland, Ghana, Kenya, Uholanzi, Philippines, Sweden, Afrika Kusini, Marekani, Australia, Russia, Scotland na Trinidad & Tobago.
Mrembo wa Thailand alinyakua nafasi ya 11 bora baada ya kumshinda mrembo wa Tanzania 2013 Happyness Watimanywa aliyeshika nafasi ya pili katika kura za (People’s Choice Awards) katika mashindano hayo.

0 comments :

 
Top