Zaidi
ya abiria mia moja wa ndege ya ATC wamekwama nchini Tanzania, baada ya
safari zao kuarishwa. Wengi wao wakielekea nchini Comoros na wengine
wakiwa katika safari za ndani, kuelekea Mtwara na Kigoma wamekwama kwa
siku mbili mjini Dar es salaam.
Abiria hao imebidi wakodiwe hoteli
ilivyo ada wakisubiri muafaka wa namna watakavyosafiri kuelekea Comoro.
Sharifu Hashim, Balozi wa heshima wa Comoro huko Chicago nchini
Marekani, anasema mambo yake mengi yamekwama kutokana na tukio hili na
hajapata uhakika ataondoka lini
Zenabal Mwarabu yeye hofu yake ni
kwa namna gani ataweza kuiwahi ndege aliyokuwa aunganishe Kisiwani
Comoro kuelekea katika kisiwa kingine cha Rarinyo.
Msawi Seifu
anasema ijapokuwa tatizo hili limetokea lakini Air Tanzania ni mkombozi
kwa wana Comoro….Lily Fungamtama, Mkuu wa Kitengo cha Biashara amesema
tayari Air Tanzania inashughulika kuhakikisha abiria wote wanasafiri
mapema kesho .
Sikukuu za mwisho wa mwaka ndilo tatizo la kukwama
kwa abiria hao,kwani marubani hawajarejea kazini tangu walipoondoka, na
walitegemewa kurejea kazini tarehe 27 mwezi huu, baada ya sherehe za
Christimas, lakini haikuwa hivyo na kusababisha sintofahamu hiyo.
Source BBC

0 comments :
Post a Comment