By Kosseyi Deogratius,sjmc
Real Madrid ni moja kati ya klabu
kubwa sana duniani.Ni klabu yenye utajiri,heshima na historia kubwa.Klabu
ambayo imetwaa ubingwa wa ulaya mara
kumi na mataji lukuki ya la liga.Kutokana na historia iliyonayo Real
Madrid,imekuwa ni kiu ya kila mwanasoka kuchezea kikosi hicho cha Santiago
Bernabeu.
Sera kubwa ya klabu hii ni
kusajili wachezaji wenye majina makubwa.Wachezaji wa kariba ya Zinedin
Zidane,Luis Figo,David Becham,Ronaldo de Lima ndio wanaohitajika Madrid kwa dau
lolote lile.
Rais wa real Madrid Ferentino
Perez ni mtu mwenye nyodo sana.Shauku yake ni kuona wachezaji aliowanunua kwa
gharama kubwa wakicheza pamoja kwenye kikosi cha kwanza.Mara nyingi makocha
wanaokwenda kinyume na mtazamo huu wa Perez,vibarua vyao vinakuwepo shakani.
Hii ndiyo sababu inayomlazimu
mtaalamu Carlo Ancelloti kuwaanzisha kwa pamoja Christiano Ronaldo,Karim
Benzema,Gareth Bale na James Rodriguez huku akifahamu kuwa timu inakosa utimamu
katika kukaba pindi inapopoteza mpira.Katika mfumo wa 4:3:3 nafasi ya kiungo
inaongozwa na Toni Kroos,Isco na James Roriguez.Kimsingi Rodriguez ni
mshambuliaji.Toni Kroos na Isco ni viungo washambuliaji kwa asili.Ukiwachukua
kwa pamoja Ronaldo,Bale,Benzema,Rodriguez,Isco na Kroos unakuwa na timu ambayo
ina wachezaji sita ambao akili yao ipo
katika kushambulia.Hapa unatengeneza tatizo katika ukabaji kwani kunakosekana
uwiano wa kukaba na kushambulia.Timu inakuwa imara katika kushambulia lakini inakuwa
dhaifu katika kuzuia.
Kwanini Ancelloti anapanga kikosi
kwa namna hii? Zipo sababu kuu mbili,ambazo kwanza ni kumfurahisha Ferentino
Perez anaetaka kuona mastaa wake wakicheza pamoja uwanjani,mastaa ambao
amewanunua kwa pesa ndefu.Lakini pili Ancelloti anatupangia timu kwa mantiki
hii kwasababu anajua La Liga ina mechi ngumu mbili ambazo ni dihi ya Barcelona
na Atletico Madrid.Katika ligi ambayo timu inaweza kushinda mechi 18 mfululizo
na kubeba ubingwa ukiwa na point 100,ni rahisi mno kupanga kikosi chenye
wachezaji sita ambao kukaba ni jukumu lao la dharura.
Ukweli ni kwamba Madrid ni hodari
mno kwenye kushambulia.Katika nafasi tano wanazoweza kupata,uwezekanao wa
kufunga magoli matatu ni mkubwa sana.Hii ndiyo silaha kubwa waliyonayo katika
kuamua matokeo ya mechi.
Real Madrid wana shimo kubwa
kwenye safu ya kiungo hasa kipindi hiki ambacho fundi Luka Modric akiuguza
majeraha.Lakini shimo hili linafukiwa na safu kali ya ushambuliaji.Kwa haraka
huwezi kuliona shimo hili.Tunahitaji timu yenye safu kali ya viungo wenye
vurugu,utimamu wa mwili na uwezo wa kukaba watuonyeshe shimo hili.Watuonyeshe
udhaifu huu unaofanana na Argentina ya Maradona ya mwaka 2010 ambae alikuwa
akitupangia kwa pamoja Messi,Aguero,Tevez,Higuain na Di maria na hatimae
wakaadhiriwa na Ujerumani kwa mabao 4:1 katika hatua ya robo fainali ya kombe
la dunia.
Je, Ancelloti ataipanga Madrid
kwa mtindo huu katika hatua ya mtoano ya
Eufa Champions League? Ni swala la muda,tusubiri tutaona.
0 comments :
Post a Comment