TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


Mbunge wa Kigoma kaskazini Zitto Kabwe, leo ameongea na wananchi wa jimbo lake kuhusu masuala ya maendeleo jimboni kwake na nchi nzima kwaujumla huku akigusia suala la maamuzi yake juu ya mstakabali wake kisiasa.
Akiwambia wananchi wake kuhusu mstakabali wake wa kisiasa Zitto alisema kuwa yeye anamwachia mwingine kijiti cha ubunge katika jimbo hilo, na yeye kuendeleza mapambano ya kisiasa kwa namna nyingine.
"lakini leo nimekuja kuwaambia ya kwamba miaka kumi inatosha, wakati wa kupisha na kukabidhi kijiti kwa mtu mwingine ili na yeye apige jaramba atusogeze mbele zaidi. Jamani nilikuja nikiwa na miaka 26 na sasa nina miaka 36, mniruhusu nikafanye mengine ili tupishe na mwingine ashike kijiti tukimbizane tupeleke maendeleo mbele zaidi. Sio kwamba kupisha kijiti ndo sintaendelea, nitaendelea kuwatetea na kuwasemea lakini kwa njia nyingine" Alisema Zitto
Pia aliongeza kuwa ameongea na wazee wake wa kijijini kwake na viongozi wa vijiji vyote jimboni kwake na wamempa baraka za yeye kufanya maamuzi yoyote yale anayoyaona yanafaa kwa mstakabali wake wa kisiasa.
Aliwasihii wananchi wake kukubaliana na atakacho amua siku za usoni, na alisema yeye bado ni mbunge wao na ataendelea kuwawakilisha mpaka pale atakapoambiwa basi.
Akizidi kufafanua kuhusu misukosuko anayoipata ya kisiasa alisema kuwa hakuna kiongozi wa kisiasa mahili asiyekuwa na  misukosuko, huku akifananisha na waziri mkuu wa China ambaye alifungwa kifungo cha ndani na chama chake mwenyewe, kwa misukosuko hiyohiyo ya kisiasa lakini mwisho wake akajakuwaongoza tena.
Akigusia kuhusu maendeleo jimboni kwake, Zitto alieleza ni jinsi gani yeye kama mwanasiasa alivyoisaidia Kigoma kutambulika na kufanya watu wapende hata kujitaja kuwa wao wanatokea Kigoma tofauti na miaka Kumi iliyopita, kutokana na hatua za kimaendeleo zilizo chukuliwa kigoma.

0 comments :

 
Top