TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


Timu ya soka Simba imemsainisha mkataba wa mwaka mmoja mshambuliaji Pape Abdoulaye Nd'aw wa ASC Niarry Tally ya Senegal, mchana huu kwaa ajili ya kukipiga kwenye kikosi hicho.
Licha ya kumsajili Ndaw anayetokea mshambuliaji Papa Niang, aliyekuja majaribio hivi karibuni kabla ya kutemwa Simba pia imemsanisha mshambuliaji mwingine Boniface Maganga aliyetokea Marsh Academy ambaye amesaini miaka miwili.
Taarifa hiyo imetumwa mchana huu kwenye mtandao wa timu hiyo na ilieleza kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa kikosi hicho Collin Frisch, alisema wachezaji hao wamepewa mikataba hiyo baada ya kufanya vizuri kwenye majaribio yao.
Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho Dylan Kerr, amevutiwa na wachezaji hao na kuutaka uongozi kuwasainisha kwa ajili ya michezo ya ligi inayoanza Septemba 12.
“Tumefikia makubaliano na kuwasainisha wachezaji hao, hivyo ni jukumu la mashabiki wetu hivi sasa kutokuwa na hofu juu ya safu yao ya ushambuliaji itakuwa ikiongozwa na wachezaji hao pamoja na washambuliaji wengine” ilisema taarifa hiyo.
Hata hivyo, Mkuu wa Habari na mawasiliano wa timu hiyo, Haji Manara ambaye alithibitisha timu yake kuwasainisha wachezaji hao, huku akikataa kusema ni kiasi gani wametoa kupata saini za wachezaji hao.
Manara, alisema dau la wachezaji hao imebaki kuwa siri ya kati yao na wachezaji wenyewe.
“Kocha alikuw anakosa washambuliaji mahiri, lakini kupitia usajili huu wa Nd'aw na Maganga, tutakuwa tumemaliza kila kitu sasa ni jukumu la kocha kuhakikisha tunafanya vizuri.
“Sala la kiasi gani tumetumia kuwapata wachezaji hawa ni siri kati yetu na wachezaji wenyewe, hivyo watu waelewe kuwa Simba imewasainisha wachezaji hao” alisema Manara.
Manara, aliendelea kusema hawezi kumzungumzia mshambuliaji wa Burundi Kevin Ndayisenga na kusema anawazungumzia wachezaji waliosainiwa na Simba.
Ndayisenga, alitajwa kujiunga na kikosi hicho kwa dau la Sh. milioni 130, baada ya awali mchezaji huyo kukataa ofa ya Simba Sh, milioni 110.

0 comments :

 
Top