TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


LEO mgombe urais kupitia UKAWA kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa amesema kuwa Mtatiro anafaa kuwa mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Segerea na kuwa msimamizi wa vipaumbele 11 vya serikali yake endapo atashinda uchaguzi huu ambao anaimani atashinda.

Aliyasema hayo alipokuwa akihutubia katika mkutano wa jimbo la Segerea, ambako alivitaja vipaumbele vyake kuwa ni, kufuta michango na ada kuanzia chekechea hadi chuo kikuu, kukusanya kodi bora na rafiki kwa wajasilia mali wadogo wadogo, kuunda tume ya kutatua migogoro, kupunguza kodi za mishahara ya wafanya kazi, kuboresha maslahi ya polisi na usalama, kupunguza foleni ya magari kwa jiji la Dar es salaam.

Aliongeza kuwa atatatua kero za boda bod, mama ntilie na wafanya biashara wadogowadogo, kukuza michezo na sanaa, kuunda tume ya kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji, kuanzisha kituo cha kushughulikia matatizo ya wannchi kwa kila mkoa, kutengeneza mkakati wa kutatua kero za maji kwa nchi nzima. Pia aliwataka wannchi kukubari kuwa mda wa mabadiriko umefika.

“nimezunguka katika mikoa 23, kila mkoa unataja mabadiliko tu, si mjini na si vijijini. Kila mtu yuko tayari kwa mabadiliko. Nataka mabadiliko hasa kwenye elimu ili vijana wetu wawe na ushindani katika soko la ajira duniani. Ninacho wasisitiza ni kupiga kura kwa wingi na kuhakikisha mnalinda kura zenu” amesema Lowassa.

Kwa upande wake Mtatiro alisema kuwa irani ya UKAWA ndio suluhu ya kero zote za wananchi, hivyo wannchi hawana budi kuipa kuara yandio UKAWA kuanzia udiwani ubunge hadi urais.

Lowassa amefanya mikutano mine ndani ya Dar es salaam, ikiwa ni Jimbo la Segerea, jimbo la Temeke, jimbo la Ubungo na jimbo la Kawe ambako watu wengi walijitokeza kumsikiliza sera zake na akiwanadi wagombea ubunge na udiwani katika majimbo hayo.



Mtatiro akiwa na aliyetangaza nia ya ubunge kupitia CHADEMA lakini baada ya makubaliano ya UKAWA amekubali kumuachia Mtatiro kupitia CUF jimbo la Segerea

Makongoro Mahanga, akimuombea kura za ushindi Mtatiro kwa wananchi, ili awe mrithi wake


0 comments :

 
Top