Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh Kenani Kihongosi amemkabidhi fedha Mwananchi Bi Aisha ambaye alitapeliwa na vijana wawili toka mwezi wa 2 mwaka 2019 Kiasi cha shilingi Milioni Nne na Elfu Kumi (4,010,000/=)
Mwananchi huyo alifika ofisi ya mkuu wa Wilaya na kueleza malalmiko yake kwa Serikali ndipo hatua zilipoanza kuchukuliwa kwa kushirikiana na wanasheria wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Jeshi la polisi wilayani Arusha.
Watuhumiwa walikiri kumlaghai mwananchi huyo na walikubali kulipa,fedha hizo na kukiri kwa maandishi kuwa hawatorudia tena na watakwenda kufanya shughuli halali na kuwa Raia wema.
Mkuu wa Wilaya Amesema Arusha sio mahali salama kwa matapeli kwani watashughulikiwa bila huruma amesisitiza wananchi kuwa wazalendo na KUITUMIKIA nchi yao na kuacha vitendo vya utapeli.
Mwisho Amesema wananchi wazidi kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo. BOFYA HAPA KUSOMA MENGI ZAIDI
0 comments :
Post a Comment