Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amesema muamko wa wadau na taasisi zilizojitokeza katika kusaidia michuano ya kombe la mapinduzi imeonesha uzalendo kwa nchi yao pamoja na kuyaenzi mapinduzi ya mwaka 1964.
Mhe. Tabia ameyasema hayo wakati akipokea vifaa mbali mbali vya michezo kutoka kwa mdau wa michezo Zanzibar Mohamed Ibrahim (Razalee) katika ukumbi wa wizara hiyo Migombani.
Amesema michuano ya kombe la mapinduzi ya mwaka huu imekuwa ya aina yake ambayo inatoa fursa kwa Tanzania kuonesha vipaji vyao.
Ameitumia fursa hiyo pia kuwashukuru wadau wote waliojitokeza kuchangia michuano hiyo na kuendelea kutowa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuchangia ili mashindano hayo yaweze kuwa na mvuto zaidi na kuwahamasisha wananchi kushiriki kutizama kwa wingi.
Kwaupande wake mdau wa michezo Razalee amesema ataendelea kutoa msukumo wa kuisaidia michezo hapa nchini.
Amesema muelekeo wa michuano hiyo unatoa hamasa ya kuendeleza ushirikiano zaidi katika michezo ambao utasaidia kuimarisha mshikamano wa Tanzania bara na visiwani.
Mbunge wa jimbo la kawe askofu Gwajima amesema amevutiwa kuona michuano hiyo imebeba hamasa kubwa na kuahidi kutoa ushirikiano wa kuichangia.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na kombe, jezi, mipira 10, viatu kwaajili ya mchezaji bora wa kila timu na firimbi. BOFYA HAPA KUSOMA MENGI ZAIDI
0 comments :
Post a Comment