TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Bondia Mada Maugo maarufu kama ‘King Junior’, juzi amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Bondia huyo ambaye anapigana uzito wa kati, alikabidhiwa kadi jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Wakili Mabere Marando kwenye sherehe za kuchangia kampeni za udiwani Kata ya mianzini. Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhiwa kadi hiyo Maugo alisema ameamua kujiunga na Chadema baada ya kuvutiwa na sera za chama hicho na kwamba siyo mambo mengine.
“Mimi ni kijana mpenda maendeleo, leo nimeamua kujiunga na Chadema kwa ridhaa yangu mwenyewe baada ya kuvutiwa na sera za chama hiki,” alisema Maugo.
Alisema, “Kupitia uwepo wangu ndani ya Chadema nitatumia nafasi hii vizuri kwa kushirikina na vijana wengine ili kuhakikisha tunatafuta maendeleo na ukombozi wa nchi yetu.”

0 comments :

 
Top