TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Mhe PAUL MAKONDA ATANGAZA MATOKEO YA KURA DODOMA THELUTHI MBILI YA ZNZ IMEKOSEKANA
Mchana huu kabla ya kuahirishwa bunge, Makonda alimwomba Makamu mwenyekiti Bunge, ili apate kunyoosha habari iliyopotoshwa mtandaoni, ile inayohusiana na kuundwa kwa Kamati ya mashauriano kama ilivyotangazwa na Sitta asubuhi kuhusu kuwahoji wale waliopigia kura za Hapana vifungu vyote kutoka upande wa Zanzibar!
Huku ikijulikana wazi kwa kila mtanzania kwamba mtaji wa 2/3 wa kuiamua Katiba hiyo umelalia Zanzibar, kwa kuundwa kwa Kamati ya mashauriano, palitaka kujengeka taswira ya kwamba, pengine kuna njama za kuwatisha ama kuwarubuni kwa kuwamwagia vishawizi zaidi ili wajumbe hao hatimaye walainike na kuwa na uchaguzi mbadala!
Lakini kwa ufafanuzi wa Makonda, pasipo yeye kujitambua, amejikuta akitangaza matokeo ya kura hiyo kabla ya wakati wake!
Makonda amesema kuwa ni utaratibu wa bunge hilo ambao uko ki kanuni kabisa, ambapo alinukuu kanuni inayosema, "endapo 2/3 haikufikiwa katika baadhi ya ibara fulani, wajumbe waliopiga kura ya hapana kuvikataa vifungu hivyo, basi wajumbe hao wataitwa mbele ya Kamati hiyo ya mashauriano (ambayo iko ki kanuni siyo ki dharura).
Na baada ya mashauriano ya ndani ya Kamati hiyo kukamilika, wajumbe hao watapatiwa fursa nyingine ya kuzipigia kura Ibara hizo! Na kama wataendelea kupiga HAPANA, basi vifungu ama ibara hiyo italazimika kuondolewa ndani ya Katiba!
Ndipo yalipo mashaka ya Bw Sitta, kwamba, "Je, hiyo HAPANA ya wajumbe hao ni dhidi ya vifungu vyote, au baadhi tu ya vifungu!" Kwa mujibu wa Sitta, wajumbe hao hawakusomeka, ndiyo maana wataitwa mbele ya kamati ya mashauriano hivyo kwamba utaratibu huo upate kuchukua mkondo wake!
Kwahiyo, kwa maelezo hayo ya Bw Makonda, yatosha kusema hivyo kwamba, katutangazia rasmi kabla ya matokeo halali, kuwa Theluthi mbili, 2/3 ya Zanzibar imeleta mgogoro, Hapana za Wajumbe hao wazanzibar zimekwamisha rasimu hiyo, na ndiyo maana, kwa mujibu wa kanuni zao kama zilivyoelezwa naye hapo juu, inabidi waitwe, washauriwe, walau kama wataendelea na msimamo wao hata baada ya kuhojiwa mara ya pili, basi kama ni vifungu au ibara itabidi viondolewe, na kama ikiwa hapana kwa katiba nzima, sijui kama ndiko kukwama kwenyewe!
Lakini zile Hapana za SIRI ambazo hazina majina ya wapiga Kura, na zile za Medina na Apollo India watahojiwa vipi hawa na Kamati hiyo ya mashauriano?
Unasikia? Mwendawazimu akikufukuza ukamkimbia, usikimbie kwa kumtega mgongo moja kwa moja! Uende mwendo wa kugeukageuka manaake bila hivyo, utajikuta kwa bahati yako nzuri, ukanusurika rungu la kichwa huku likibaki limeuchakaza mgongo wako!
Theluthi mbili hakuna! Kwa mujibu wa Makonda! Mashauriano lazima yafanyike kuokoa jahazi!

0 comments :

 
Top