TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

JOE HART FITI KUANZA LEO LIGI YA MABINGWA

Kipa namba moja wa Manchester City, Joe Hart anatazamiwa kuanza katika mechi ya leo ya Ligi ya mabingwa ya Ulaya dhidi ya Roma na amesema kwamba ana imani kubwa ya kurudisha uhaminifu wake kwa kocha wake, Manuel Pellegrini.
Hart wakati wa moja ya mechi zake za Ligi ya mabingwa Ulaya

Pelegrini amemuweka benchi Hart katika mechi mbili mfululizo, jambo ambalo limezua maswali mengi kwa mashabiki wa timu hiyo, juu ya uwezo wa kipa huyo na hofu zaidi ikiongezeka baada ya Liverpool kuonyesha nia ya kumnasa ‘Short-stopper’ huyo.
Hart ambaye ametwaa tuzo ya kipa bora wa misimu mitatu mfululizo, anaonekana kushindwa kumudu presha za mechi msimu huu baada ya kuruhusu magoli mara kwa mara na kushindwa kupata ‘clean sheet’.

MSIKIE ‘THE FLYING DUTCHMAN’, VAN PERSIE.

Mshambuliaji wa Machester United, Robin van Persie amesema United ina washambuliaji hatari zaidi kiasi cha kuwaogopesha wapinzani wao.

Jezi za baadhi ya wachezaji hatari wa united zikiwa zimetundikwa Old Traford
kabla ya mechi ya Juzi dhidi ya West Ham United
Van persie aliyasema hayo wakati akijibu swali aliloulizwa na ESPN kuhusu uwezo wa washambuliaji wa United msimu huu.
 "Nadhani tunaweza kuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Kama ukiangalia wachezaji tulionao, ni wachezaji wakubwa na wenye uwezo binafsi".

Van Persie bado ana amini kuwa, kwa nguvu ya kushambulia walio nayo United, bado watafanya vizuri japo nahodha wao, Wayne Rooney alitolewa nje kwa kadi nyekundu Jumamosi kwa kumchezea vibaya mchezaji wa West Ham wakati United ilipoibuka kwa Ushindi wa 2-1.

MONEY TAKES ALL

Raheem Sterling akifurahia goli alilowafunga Arsenal Msimu uliopita

Liverpool wanajiandaa kumpa mkataba mpya utakaomlipa mshahawa wa zaidi ya mara tatu winga wao Raheem Sterling ili kumbakisha Anfield kwa muda mrefu zaidi.
Winga huyo anayewindwa na Real Madrid ya Hispania, anatarajiwa kupewa mkataba utakaomfanya alipwe pauni 100 kwa wiki, tofauti na pauni 30 kwa wiki anazolipwa sasa.




YES, BUT NOT TOO SOON.

Huenda mshambuliaji wa zamani ManchesterUnited, Cristiano Ronaldo akarejea klabuni hapo, lakini baada ya misimu miwili na zaidi kupita
Bango lililokuwa likiongozwa na ndege ya kukodi, lilipita juu ya uwanja wa santiago bernabeu wakati wa mechi kati ya Real Madrid na Vilareal.
Kocha wa mshambuliaji huyo wa sasa, Carlo Anceloti ametupilia mbali tetesi zote za CR7 kuondoka Real Madrid msimu ujao na kusema Ronaldo atabaki Santiago bernabeu kwa zaidi ya misimu miwili ijayo.
                       
Kama hukusikia!
Mashabiki wa Manchester united, walikodi ndege iliyobeba bango lililosomeka ‘Njoo                         nyumbani Ronaldo’ wakati real Madrid ikicheza na Vilareal katika uwanja wa                                     Santiago Bernabeu. Ronaldo alipoona bango hilo alionekana kuwa mtu wa  hisia                                 wakati wote wa mechi.




0 comments :

 
Top