Akiwa na miaka 27 tu mwanasoka bora wa zamani wa dunia Lionel Messi amezidi kuchafua vitabu vya rekodi kwa kuweka na kuzivunja rekodi mwenyewe.
Leo hii wakati FC Barcelona ilipoikaribisha Granada kwenye dimba la Nou Camp, Lionel Messi alifunga magoli mawili katika ushindi wa magoli 6-0.
Magoli hayo mawili yamemfanya Messi atimize jumla ya magoli 401 katika mechi 524 alizoichezea FC Barca na Argentina. Hii ni rekodi mpya kwa Messi.
Magoli mengine ya Barca yalifungwa na Neymar aliyefunga matatu, na Rakitic.(P.T)
0 comments :
Post a Comment