Kama tunakumbukumbu ndugu Watanzania, kipindi wananchi wanalalamika kuhusu upandaji wa nauli za daladala kwa upande wa Dar es salaam. serikali ilikuja juu na kujetetea kuwa inataka kufanya mabadiliko ya huduma kwa kufanya iwe bora zaidi na wenye kuvutia machoni mwa Watanzania
Mimi nikiwa kama mtanzania kati ya tulio aidiwa huduma hiyoo naona kama SUMATRA wanawachezea na kuwafanya Watanzania hawana akili na ni wakuwadanganya tu.
Na kwa upofu wa Watanzania wao wamesahau kabisaa kwa kudanganywa huko, kwani hawalalamiki tena ongezeko la nauli hiyo ambayo haiendani na ubora wa huduma iliyo aidiwa.
Kama mkweli kulikywa na lengo la kuboresha huduma, kwanini wasingefanya uboreshaji huo ndipo wapandishe naulii..?
Kwa kumbukumbu zangu hii sio mala ya kwanza kwa watanzania kupewa sababu zisizo na kichwa wala mkia na Watanzania wenyewe wanakuwa hawana neno pale tu wanapopewa aina fulani ya sababu hata kama wanaona sababu hizo hazina uimara wowote ule.
Hivi ndo kusema sikuhiuzi uizi unakuwa unahalalishwa tu, kwasababu jinsi ya ulipaji wa nauli zenyewe mimi naona kama ni uizi kabisa. kwanini SUMATRA wasingeweka ulipaji wa nauli kwa umbali fulani wa kolometa...? kwanini mtu anaye panda gari kwa kilometamoja tu naye alipe 400( mia nne ) ?
Serikali waoneeni huruma wananchi wenu, vipato walivyonavyo haviwatoshi kulipia ghalama mnazo waletea.
Wananchi wakiwaletea malalamiko yao juu ya kuwatetea katika vibarua vyao wala hamuwasikilizi, ila mabepali wakileta yao ndo wa kwanza kusikilizwa hatakama inaonekana wanawakandamiza wenginee
WATANZANIA TUBADILIKE, TUWE TUNATAMBUA MAHITAJI YETU NA KUWEZA KUYATETEA BILA UWOGA.
Home
»
»Unlabelled
»
SUMATRA WAWAFANYA WATANZANIA MIDOLI YA KUCHEZEA
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment