TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

pope
Vatican. Papa John Paul II atapewa Utakatifu baada ya Vatican kuthibitisha muujiza wa pili inayosema ulitokea kutokana na sala zake.
Baba Mtakatifu wa sasa Francis I amehakiki muujiza huo, akisema unatoa nafasi kwa John Paul aliyezaliwa Poland kutangazwa Mtakatifu baadaye mwaka huu.
John Paul II, aliyezaliwa Karol Józef Wojtyła mwaka 1920, alikuwa kiongozi wa kiroho wa waumini zaidi ya bilioni moja wa Kanisa Katoliki toka mwaka 1978, mpaka alipofariki mwaka 2005.
Vile vile, Francis I ametangaza pia kumpa utakatifu Papa mwingine, John XXIII, ambaye aliongoza kanisa Katoliki toka mwaka 1958 hadi 1963

0 comments :

 
Top