TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

kamanda wa kanda maalumu ya Dar es salaam  Suleiman Kova, amefichua sili ya mafdanikio ya usalama wakati wa kipindi chote cha ugeni mkubwa ukliokuwepo Tanzania ukiwa ni ule wa marais 14 kutoka nchi mbali mbali, wake za mararais pamoja na ule mkubwa zaidi wa Rais Barack Obama,
akifafanua leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Kova alisemakuwa katika upande wa ulinzi katika kipindi chote hicho cha ugeni wamefanikiwa kiasi kikubwa saana kutokana na Mchango mkubwa wa waandishi wa habari kwa kutoa maelekezo vizuri kwa wananchi ninni wafanye wakati wa ugeni huo utakapokuwa nchini
"navipongeza vyombo vya habari havikuandika habari hasi kuhusu ugeni huo, bali viliandiuka habari chanya juu ya ugeni huo kitu kilichosaidia wananchi kuwa watulivu kwani vyombo vya habari vinanguvu katika kuwashawishi uma nini wafanye" alisema kamanda Kova.
aliongeza pia kuwa ushilikiano na vikundi vingine kama vile, Polisi jamii, JWTZ, fire, usalama wa taifa ilikuwa ni chachu ya mafanikio ya ulinzi na usalama hapa Dar es salaam.
kamanda Kova alikili kuwa kumbe kutumia elimu ya kuwahamasisha watu ni bora zaidi kuliko kutumia mabom na njia nyingine yoyote ya amli.
aliongeza kuwa jeshi la polisi limejipanga vyema kuhakikisha ulinzi na usalama pamoja na usafi wa jiji kubaki kama iulivyokuwa wakati wa ugeni
"tutatumia polisi jamii ili kulinda maeneo yote yabaki masfi, kazi yao itakuwa kuwakamata wale wote wanao tupa takataka ovyo na kuwatoza faini, hali hii itafanya jiji letu ling'ae" alisema Kova
alimalizia kwa kusemakuwa hata ujambazi na ualifu wowote ule ulitoweka katika kipindi hicho na pia aliwapongeza wananchi kwa utulivu wao.

0 comments :

 
Top